Baadhi ya
wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao baada ya mwanachama wao
Lawrence Masha kujivua uanachama na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa kama sababu
za kujivua kwake.
Kwenye
kurasa zao mbali mbali za mitandao ya kijamii Mbunge wa Arusha Mjini Godbless
Lema, ameandika ujumbe akisema safari ya kupigania usawa na haki ni safari
ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo ni aibu kwani kuna
wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa safari.
“Lawrence
Masha , struggle ya kupigania usawa,haki na demokrasia, ni safari ndefu na ngumu
,wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na wanawake imara
wanaendelea na safari,sio uamuzi mbaya uliochukua ila ni uamuzi wa aibu .
Utajua baadaye na sio sasa”, ameandika Godbless Lema.
Naye Mbunge
wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema wanajua sababu
za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo
wanaheshimu mamuzi yake.
“Tunaojua
sababu za Masha kutoka CHADEMA zile kwenye barua yake tunajua ni danganya toto,
tunajua sababu na tunaziheshimu. Kuthibitisha kuwa CHADEMA imejipanga kuingia
ikulu, angalia takwimu za ushindi wa madiwani na wabunge nchini kuanzia 1995
hadi sasa. Ikulu ni suala la muda, tena si mrefu”, ameandika Joshua Nasari.
Pia Katibu
Mkuu wa chama hiko Vicent Mashinji aesema Masha kuondoka CHADEMA ni haki yake
kisheria, lakini ni vyema akaweka wazi ukweli wa sababu za yeye kuondoka.
“Mheshimiwa
Masha ana haki kisheria, namtakia heri, lakini lazima auambie umma nini hasa
kilichotokea”, ameandika Mashinji.
Lawrence
Masha hapo jana ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA akisema chama hiko
hakina malengo ya kushika dola, kama ambavyo malengo ya vyama vya upinzani
huwa.
0 Comments