Klabu ya Singida United Football Club kupitia kwa Mkurugenzi wake Ndg. Festo Sanga ametangaza habari njema kwa Klabu hiyo kwa kuingia mkataba wa mafanikio na mnono wa miaka miatatu (3) wa kuanzishwa kwa SINGIDA UNITED TV kupitia Azam Tv.
Akizungumza kwa furaha, Mkurugenzi
huyo, amesema: “Tunawashukuru Uhai
production wanaoendesha Azam Tv kwa kukubali kuanzishwa kwa kipindi cha Singida
United Tv kitakachokuwa kinarushwa kupitia Azam Tv. Ni mafanikio ya kujivunia
kuona kila mkakati tunaoupanga unafikia maleng.
Tunaendelea kuwaomba watanzania na
wadau wa mpira kuwa tuungane kuleta mabadiliko ya uendeshaji wa vilabu vyetu na
zaidi soka kwa ujumla. “Pia kuanzishwa kwa SINGIDA UNITED TV ni moja ya njia ya
kuwatangaza wadhamini wetu ambao wamewekeza kwenye club yetu.” Alieleza Sanga.
Mtendaji Mkuu wa Uhai
Production, Ndg. Tido Mhando akimkabidhi
mkataba walioingia leo na Singida United, ndg. Festo sanga Mkurugenzi wa
Singida United Football Club.
0 Comments