Staa wa muziki nchini jumanne ya
Septemba 19 mwaka huu amemaliza maswali ya mashabiki wa muziki nchini na
Watanzania kwa ujumla kujua ukweli kuhusu mtoto ambaye mwanamitindo Hamisa
Mobetto amemzaa kama ni wake au sio wake.
Jibu la Diamond ni NDIYO NI WANGU na
hivyo Watanzania kupata jibu la swali walilohitaji kupata majibu kutoka kwa
Diamond Platnumz.
Pamoja na hilo Diamond ametoa video
ya mtoto huyo ambaye kwa mujibu wake jina alilotoa kwa mtoto ni Dayllan lakini
mama wa mtoto ameamua kumpa mtoto jina la baba wa Diamond ambalo ni Abdul.
0 Comments