Klabu ya Yanga imepatwa na msiba mzito wa baba yake mzazi na
kocha mkuu wa klabu hiyo, Mzambia George Lwandamina.
Kocha wa Yanga, George Lwandamina
Taarifa hiyo
imethibitishwa na Afisa habari wa klabu hiyo Dismas Ten na kusema kuwa
ni kweli kocha wao amepatwa na msiba wa baba yake mzazi huko kwao Zambia na
tayari wameshafanya mpango wa kumsafirisha Lwandamina kwenda kuhudhuria msiba
huo.
“Lwandamina ameondoka leo nchini Tanzania kuelekea nyumbani
kwao Zambia kwa ajili ya mazishi ya baba yake, ila akifika huko ndiyo tutaweza
kujua tarataibu za mazishi kwa kuwa shuguli zote zinafanyikia huko kwao”,.
Hata hivyo awali taarifa za kuondoka kwa kocha huyo nchini
Tanzania zilieleza kuwa kuna matatizo ya kifamilia.
Singida Blog na laurentcomputercentre.com inatoa pole kwa kocha Lwandamina na klabu ya
Yanga kwa ujumla.
Na Laurent Mpoma


0 Comments