Follow us

IJUA SAFARI YA ARTETA NDANI YAARSENAL

Tangazo

 


IJUA SAFARI YA ARTETA NDANI YAARSENAL

Klabu yaArsenal baada ya kuwa na mapito mbalimbali ya kutokuwa na nafasi nzuri ndani yaEPL hataimaye waliamua kumsajili aliyekuwa mchezaji wao Mikel Arteta ambayempaka sasa anakionoa kikosi hicho. Na haya hapa ndiyo mafanikio yake.

Mikel Artetaalizaliwa 1982 mwezi Machi Hispania ambapo alicheza katika vilabu mbalimbaliwakati akiwa kijana. Alicheza vilabu kama vile Barcelona, PSG, Rangers, RealSociedad, Everton 2005 kwa mkopo ambapo baadae alijinga nao moja kwa moja.

Wakati akiwakatika klabu ya Everton alifanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora mara mbiliwa msimu klabuni hapo. Baada ya kufanya vizuri na The TOFFEES Mikel alisainiwana Arsenal kwa dau la Euro 10m mwaka 2011 chini ya kocha mkuu Arsene Wenger naakafanikiwa kuchukua mataji ya FA, na kuwa nahodha wa kikosi hicho kuanziamwaka 2014 hadi 2016 pale alipostaafu.

Lakini licha ya kuwa na kiwango kizuri Mikel Arteta hakuwahi kuichezea timu ya Hispania ya wakubwa. Na baada ya kustaafu kucheza soka kocha huyo aliteuliwa kuwa kocha msaidizi katika klabu ya Manchester City ambapo kocha mkuu wake alikuwa ni Pep Guardiola hadi sasa. Jisajili meridianbet ubashiri mechi za leo.

Mnamo mwaka 2019 Arteta alirejea ndani ya The Gunners na kusajiliwa kama kocha mkuu ambapo ilikuwa ni tarehe 20 mwezi Desemba ambapo ndani ya msimu huo huo alifanikiwa kuchukua taji la Kombe la FA mbele za Chelsea.

Hivyo basi baada ya kubeba taji hilo ilimfanya Arteta kuwa mchezaji wa kwanza kushinda taji la FA kama nahodha na kocha wa The Gunners. Na hiyo ikawafanya wafikishe makombe 14 ya FA kushinda klabu yoyote ile Uingereza.

ARSENAL NA REKODI YAO

Arsenal chini ya Arsene Wenger inaendelea na rekodi yao za kuwa timu pekee Uingereza ambayo ilichukua Taji la EPL msimu wa 2003/2004 wakiwa hawajapoteza mechi yoyote wakiwa wameshinda mechi 26 na sare 12 pekee na kuchukua ubingwa huo wakiwa pointi 11 mbele zaidi ya Chelsea ambaye alishika nafasi ya pili.

ARSENAL KWENYE LIGI KUU

Baada ya Arteta kuichukua Arsenal chini ya Unai Emery  msimu wa 2019-2020 The Gunners baada za msimu kuisha wlaishika nafasi ya 8, wakati msimu uliofuatia wa 2020-2021 alishika nafasi hiyo hiyo. Kutokana na mwenendo huo presha ilizidi kuwa kubwa kwa kocha huyo wa Kihispania.

Kelele zilikuwa nyingi sana mpaka mashabiki wengi wakawa wanataka kocha huyo afukuzwe kutokana na kiwango kibovu ambacho timu yake ilikuwa ikikionyesha. Lakini kuna methali ya kiswahili inasema kuwa “Mvumilivu hula mbivu” Arsenal walimvulia sana Arteta.

Msimu unaofuata wa 2021/2022 Washika mitutu wa London walishika nafasi ya 5 ambayo iliwafanya washiriki Europa mabayo nayo hawakufika mbali walitolewa na FC Barcelona ambapo msimu huo City alichukua taji la ligi kuu.

The Gunners walivumilia na kufanya usajili mkubwa kwa kuwekeza kwa vijana ambapo baadhi ya wachezaji waliosajili chini ya Arteta ni kama vile, Martin Odergaard, Ben White, Leandro Trossard, Pablo Mari na wengine kibao.

Msimu wa 2022/2023 Arsenal ya Mikel Arteta ilizidi kuwaka moto sana na hatimaye kumaliza nafasi ya 2 kwenye msimamo wa EPL chini ya vijana wa Pep Guardiola baada ya kufanya makosa kidogo ambayo yalimfanya akose ubingwa.

Na sasa yupo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi huku nafasi ya pili ikiwa ni ya Manchester City, ya kwanza ikiwa ni ya Liverpool huku wakiwa wamepishana pointi moja moja. Yani kila timu ina nafasi kubwa za kuchukua ubingwa huo ikichanga karata zake vizuri.

Pia Arsenal msimu huu bado haijafungwa na timu kubwa, kwani mpaka sasa amemfunga Manchester City, Manchester United, na Liverpool kwenye mechi za kwanza.

ARTETA NA LIGI YA MABINGWA (UEFA)

Ina fahamika kuwa Arsenal kwenye zile timu nne bora za Uingereza ndiyo timu pekee ambayo haijawahi kuchukua taji la ligi ya Mabingwa yani UEFA, huku mara ya mwisho

kufika fainali ilikuwa mwaka 2005/2006 ambapo kwenye hatua za mtoano walifanikiwa kuwafunga Real Madrid, Juventus, na Villarreal chini ya Wenger.

Arsenal ilifungwa na Barcelona 2-1 na kupoteza fainali hiyo na hiyo ikawa ndiyo mara ya mwisho kwa The Gunners kufika hatua hiyo kwenye ligi ya Mabingwa barani Ulaya tena.

Na sasa Arsenal kwenye UEFA alipangwa kundi moja na PSV kutoka Uholanzi, RC Lens kutoka Ufaransa, na Sevilla kutoka Hispania. Arteta aliongoza kundi hilo B baada ya kupata pointi zake 13, akishinda mechi zake 4, sare 1, na kupoteza mara 1.

Baada ya kuongoza kundi hilo hatua ya 16 bora Arteta alipngwa na FC Porto ya Ureno ambapo alianzia ugenini na akapoteza kwa bao 1-0. Je kwenye mechi ya marudiano akiwa pale Emirates anaweza kupindua meza na kwenda Robo Fainali ya mabingwa?. Je Arteta na Arsena yake baada ya msimu uliopita kukosa makombe yote msimu huu anaweza kuambulia chochote?

Post a Comment

0 Comments