Follow us

AHMED ALLY: KIPIGO CHA TANZANIA PRISONS KISITUVURUGE SIMBA

Tangazo

 


https://singidamatukio.blogspot.com/2024/03/ahmed-ally-kipigo-cha-tanzania-prisons.html

AHMED ALLY: KIPIGO CHA TANZANIA PRISONS KISITUVURUGE SIMBA

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, AhmedAlly amesema kuwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wanapaswa kushikama nakuendelea kuisapoti timu yao na wachezaji wao licha ya kupoteza mchezouliopita.

Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Tanga kwa ajili yamchezo wao dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho Jumamosi katika Dimba laMkwakwani huku Mnyama akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi yaTanzania Prisons kwa kipigo cha bao 2-1.

“Matokeo ya Prison mimi mwenyewe nimeumia sana, nilikuwakwenye hali mbaya mno ila sikulia. Nimesikitika, mechi ilikuwa ngumu ile. Hatanikilia hakuna shida kwa sababu naililia simba yangu lakini sina muda wa kulia.

“Haya ni maumivu yetu sote asijitokeze mtu akajimilikishamaumivu kuwa ni yake peke yake kwa sababu haya ni maumivu yetu sote. Ukitumiamuda mwingi kutafuta mchawi unapoteza focus ya kujiandaa na mchezo ujao.

“Mechi ya Coastal ni ngumu vibaya mno, wale jamaa sio wakawaida, wana hatari sana. Lazima tushikamane, la sivyo tutapoteza mchezo wapili mfululizo na tutaanza kukimbiana hapa,” amesema Ahmed Ally.

 

Post a Comment

0 Comments