Follow us

TABORA UNITED YAAMBULIA 4G KUTOKA KWA SIMBA

Tangazo

 


WENYEJI Tabora United wakiwa Uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi wamekubali kupoteza pointi tatu mbele ya wapinzani wao Simba ndani ya dakika 90 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulikuwa ni kiporo.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Tabora United 0-4 Simba wakikomba pointi tatu ugenini.

Mabao ya Simba yamefungwa na Pa Omary Jobe dakika ya 19, Sadio Kanoute dakika ya 36, Che Malone dakika ya 60 na Fredy Michael dakika ya 87.

Mchezo wao uliopita ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ubao ulisoma Mashujaa 0-1 Simba.

Katika mchezo uliopita bao la ushindi lilifungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 16 kwa mkwaju wa penalti.

Simba inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 12 nafasi ya tatu huku vinara wakiwa Yanga na pointi zao 34 baada ya kucheza mechi 13 sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 31.

Post a Comment

0 Comments