NI NIGERIA NA IVORY COAST FAINALI AFCON JUMAPILI ABIDJAN
Tangazo
Ilianza
Nigeria kuitupa nje Afrika Kusini kwa mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare ya
1-1 ndani ya dakika 120 Bouaké.
Beki wa PAOK
ya Ugiriki, William Paul Troost-Ekong alianza kuifungia Nigeria kwa penalti
dakika ya 67, kabla ya kiungo wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Teboho
Mokoena kuisawazishia Bafana Bafana dakika ya 90.
Katika
mikwaju ya penalti kipa Stanley Bobo Nwabali wa Chippa United ya Afrika Kusini
aliibukia shujaa kwa kuokoa mikwaju ya Mokoena na Evidence Makgopa, huku za
Mihlali Mayambela na Mothobi Mvala pekee zikimpita.
Waliofunga
penalti za Nigeria ni Teremas Moffi, Kenneth Omeruo, Troost-Ekong na Kelechi Ịheanachọ,
huku Temitayo Aina pekee akikosa.
Baadaye
Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan, bao la mshambuliaji wa
Borussia Dortmund, Sébastien Haller dakika ya 65 likatosha kuwapeleka wenyeji,
Ivory Coast Fainali wakiichapa DRC 1-0.
Sasa Ivory
Coast itakutana na Nigeria katika ‘Bonge la Fainali’ Jumapili Uwanja wa Félix
Houphouët-Boigny Jijini Abidjan yakiwa ni marudio ya mchezo wa Kundi A mwanzoni
mwa mashindano Super Eagle ikiwatandika Tembo 1-0.
Afrika
Kusini na DRC zitacheza mechi ya kuwania nafasi ya tatu Jumamosi.
0 Comments