Follow us

KINDA MTANZANIA WA MIAKA 12 ANG’ARA URUSI

Tangazo

 

KINDA MTANZANIA WA MIAKA 12 ANG’ARA URUSI

NI wazi kuwa Tanzania imeng’ara baada ya mwakilishi pekeekinda Mtanzania, Harrith Chunga Misonge mwenye umri wa miaka 12 kuwa gumzo.

Misonge mkazi anaiwakilisha Tanzania kwenye michuano yaPhygital Football for Friendship akiwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Masharikina Kusini mwa Afrika.

Mwakilishi mwingine ni mtoto kutoka Afrika ya Kati lakinihajang’ara kama Misonge ambaye amepewa nafasi ya uongozi katika kiongozi.

Viongozi wa watoto hao wamemsifia kwa uwezo wa kucheza sokalakini pia ni kiongozi na wakati wa ufunguzi yeye aliwaongoza wenzake.

Ni mtoto mtaratibu mwenye kipaji na leo ni Mtanzania mwakilishiwa Afrika barani Ulaya kwenye michuano mikubwa ya watoto kujenga umoja, unduguna urafiki lakini kujifunza mambo mengi yakiwemo ya maisha.

Russia imeona kuna nafasi ya kuwasaidia watoto kuungana nakuiunganisha dunia kutumia watoto.

Harrith, mwanafunzi katika shule ya Aghakhan anakuwa sehemuya mwanga kwa watoto wa Kitanzania kuwa INAWEZEKANA.

Mwaka jana alifanya vema katika michuano ya Gothia nchini Sweden na sasa nyota yake inag’ara hapa katika jiji la Kazan.

Post a Comment

0 Comments