IVORY Coast ni mabingwa ushindi wapya wakionyesha maajabu yao kwa kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa fainali uliokuwa ni wa kuvuja jasho na akili nyingi.
Baada ya
dakika 90 wenyeji Ivory Coast waliibuka kwa ushindi wa mabao 2-1 Nigeria katika
fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2023.
Ikumbukwe
kwamba mabingwa watetezi walikuwa nj Senegal waliokwama kutetea taji hilo Ivory
Coast.
Mabao ya
Ivory Coast ambayo ilipenya ikiwa ni best looser iliwashangaza Nigeria kwa
mabao ya Frank Kessie dakika ya 62 na la ushindi lilifungwa na Sebastien Haller
dakika ya 81.
Ivory Coast
mabingwa AFCON 2023 ikiwa ni mara ya tatu kutwaa taji hilo kubwa Afrika.
Licha ya
nyota Ekong mapema kuwatanguliza Nigeria dakika ya 37 halikutosha kuwapa taji
hilo katika mchezo wa fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa ñdani ya uwanja.
Ilikuwa kazi
kubwa na mwisho imehitimshwa huku Afrik Kusini wakiwa ni washindi watatu kwenye
AFCON hiyo.
0 Comments