Joto la
fainali ya AFCON kule nchini Ivory Coast mwisho wake ni leo ambapo Nigeria
atakipiga dhidi za Ivory Coast majira za saa 5:00 usiku huku kila mtu
akiisubiria kwa hamu mechi hiyo baada za michuano hii kunoga zaidi kwani
upinzani ulikuwa mkubwa sana.
“Waswahili wanasema ukistaajabu ya Mussa
utayaona ya Firauni” hasa baada ya wale ambao walitarajiwa kufika mbali
wakatolewa kwa kushangazwa akiwemo Egypt ambae ni bingwa mara 7 wa michuano
hii, Ghana ambaye alisumbua Kombe la Dunia, Morocco ambao alikuwa ni mshindi wa
4 Kombe la Dunia lilipoita, Senegal ambae alikuwa ni bingwa mtetezi wa Kombe
hili la AFCON, Algeria na wengine wengi.
Ikumbukwe
kuwa Nigeria ambao kwasasa wapo chini ya kocha mkuu Jose Peseiro ni washindi wa
Kombe hili mara tatu ambalo walilichukua mwaka 1980, 1994 na mwaka 2013, huku
Ivory Coast chini ya kocha mkuu kwasasa Emerse Fae wao wakichukua kombe hili
mara mbili pekee Mwaka 1992, na 2015.
Ndugu mteja
ukiendelea kuchanganua nani wa kumpa ushindi kwenye Fainali meridinabet
wanakwambai cheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile Poker, Roullette,
Aviator, Sloti na mingine kibao sasa. Ingia na ucheze.
Na sasa ndugu
mteja wa Meridianbet tunaenda kuangalia ni kwa namna gani timu hizi mbili
Nigeria au kwa jina jingine THE SUPER EAGLES na Ivory Coast kwa jina lingine
THE ELEPHANTS walivyofika kwenye hatua hiyo ya Fainali ya AFCON msimu huu
kuanzia hatua ya makundi.
HATUA YA
MAKUNDI
Kwanza
kabisa timu hizi zilikuwa kwenye kundi 1 kwenye michuano hii ya AFCON ambalo
lilikuwa ni Kundi A, ambalo lilikuwa na timu nne ikiwemo Guinea Bissau,
Equatorial Guinea, Ivory Coast pamoja na Nigeria wenyewe.
Kwenye kundi
hilo Nigeria alishika nafasi ya pili baada ya kupata pointi 7 akishinda mechi 2
na kutoa sare 1, huku The Elephants wao wakishinda mechi 1 na kupoteza mechi
mbili na kupita kwenye 16 bora kama “BEST LOOSER”
Lakini
walivyokutana wao kwa wao Nigeria alishinda mechi hiyo dakika ya 55 baada ya
kupata mkwaju wa penati ambao ulifungwa na captain wao Troost-Ekong na kuiptaia
timu yao alama 3.
HATUA YA 16
BORA
Ndani ya 16
bora sasa mambo yalikuwa ni moto zaidi ambapo kila timu ilihitaji kushind
ambapo Nigeria yeye alipangwa kukipiga dhidi ya Cameroon ambao nao walikuwa ni
moja ya timu walipigiwa upatu wa kushinda taji hili lenye thamani kubwa Afrika.
Lakini The
Super Eagles walionyesha ukubwa wao kwa kumchapa Camroon kwa mabao 2-0 dakika
90 za mchezo huku mabao hayo yakifungwa na Ademola Lookman mchezaji ambaye
anakipiga kule Atalanta ya Italia.
Wakati kwa
upande wa Ivory Coast mwenyeji wa michuano hii hatua hiyo alipangwa na na
bingwa mtetezi wa michuano hii Senegal ya Sadio Mane ambapo takribani watu
wengie walimpa nafasi kubwa Msegali kuondoka na ushindi. Lakini mechi ikawa
tofauti na matarajio ya watu baada ya kuishna 0-0 dakika 90 za mchezo na
hatimyae kwenda matuta.
The
Elephants hatimaye walitinga hatua ya Robo Fainali baada ya kushinda kwa
mikwaju ya penati 5-4 na kushangaza walio wengi na kusema kweli mpira ni dakika
90 na filimbi ya mwisho ndiyo itaamua nani ni nani.
HATUA YA
ROBO FAINALI
Kwenye hatua
hii mechi zilikuwa kali sana kutokana na timu ambazo zilikuwa zimetinga kwenye
hatua hii ya Robo Fainali kwani Nigeria yeye safari hii alikutana na Angola
ambaye alimchapa bao 1-0 ndnai ya dakika 90 za mchezo.
Ivory Coast
yeye alikipiga dhidi ya Mali ambao walionekana kuwa wabishi sana kutokana na
kikosi ambacho walikuwa nacho. Lakini vijana wa Fae walikuwa wabishi baada ya
kushinda kwenye muda wa ziada kwa 2-1 licha ya kuwa na kadi nyekundu 1.
HATUA YA
NUSU FAINALI
Nigeria yeye
alishinda kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kwenda dakika 90 kwa bao 1-1 dhidi
ya South Africa pongezi zikienda kwa Golikipa wao Nwabi ambaye aliokoa penati
tatu. Huku Ivory Coast wao wameingia Fainali baada ya kuichapa DR Congo kwa bao
1-0 dakika 90 za mchezo bao ambalo lilifungwa na Sebastian Haller.
Baada ya
kushuhudia mechi mbalimbali za AFCON 2023 sasa tamati ni siku ya Jumapili hii
ya tarehe 11 Februari saa 5:00 usiku katika Dimba la Alassane Outtara ambapo
Nigeria atazichapa dhidi ya Ivory Coast huku timu zote zikiwa na hamu ya
kuchukua Kombe hili 2023.
0 Comments