TIMU ya taifa ya Mali anayocheza kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra iliwafungashia virago wapinzani wao Burkina Faso anayocheza Aziz KI anayecheza Klabu ya Yanga.
Ndani ya
dakika 90 kwenye hatua ya 16 bora mshindi aliyetinga robo fainali ya Kombe la
mataifa ya Afrika (Afcon) ni Mali baada ya kutinga Burkina Faso mabao 2-1
katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly Ivory Coast.
Mabao ya
mchezo huo kwa upande wa Mali yamefungwa na Edmond Tapsoba aliyejifunga dakika
ya tatu na Lassine Sinayoko dakika ya 47’ huku la Burkina Faso likifungwa na
Betrand Traore 57 kwa mkwaju wa penalti akimpoteza mlinda mlango Diarra.
Kwa ushindi
huo Mali itakutana na Ivory Coast Februari 3 katika robo fainali inayotarajiwa
kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.
0 Comments