HATIMAYE bingwa mtetezi Senegal katika Kombe la Mataifa Afrika mwendo ameumaliza kwa kufungashiwa virago na Ivory Coast.
Senegal
walikuwa ni mabingwa wa 2022 wa AFCON safari yao imegota mwisho baada ya
kupoteza mbele ya Ivory Coast kwenye mchezo ambao walikuwa wakipewa nafasi
kubwa ya kusonga hatua inayofuata.
Ilikuwa ni
hatua ya 16wanaishia wakikwama kutinga robo fainali kwenye mchezo uliokuwa na
ushindani mkubwa kwa kuchezwa dakika 12.
Ikumbukwe
kwamba Januari 29 baada ya dakika 90
ngoma ilikuwa Senegal 1-1 Ivory Coast katika dakika 30 nyingine ngoma ilikuwa
ngumu kwa timu zote.
Kwenye
penalti Senegal yenye nyota Sadio Mane ilifunga 4-5 Ivory Coast ambao walitinga
hatua ya 16 bora wanakwenda robo fainali na ni wenyeji wa mashindano hayo.
Mabao
yalifungwa na Habib Diallo dakika ya 4 kwa Senegal na Franck Kessie dakika ya
86 kwa mkwaju wa penalti.
0 Comments