HUYU HAPA
MRITHI WA MIKOBA YA KLOPP LIVERPOOL
JURGEN Klopp
ataondoka mwishoni mwa msimu. Hili siyo suala la mjadala tena. It is true, Ni
kweli kabisa kuwa ataondoka. Mjadala umewefungwa.Mjadala wa sasa ni nani haswa
anaepaswa kuchukua mikoba yake?! Mtazamo wangu mimi uko kwa msaidizi wa Klopp.
Pepjin Lijnders. Huyu ndie naemuona kama mrithi sahihi wa Klopp. Viashiria vipo
vingi na tunaweza kujadili pamoja.
Awali
niliwaeleza kuhusu utamaduni wa Kocha wa Liverpool kuzalishwa kupitia Boot Room
Tradional enzi za akina Bill Shankly.
Shankly
wakati anaondoka 1974 ilikua ni mshtuko mkubwa kwa Liverpool. Na kukawa na
mipango ya kuchukua mrithi wake kutoka nje ya Liverpool.
Majina ya
Jack Charlton na Bobby Robson yalitajwa kama outiside successors wa Shankly.
But Klabu ikasema maneno haya, “ We simply dont want to lose on what Shankly
had built in his 15 years. We want continuity” Klabu ilitaka kuendeleza project
ambayo tayari imeanzishwa na Shankly.
Na hii kauli
ndio tutaitumia kumpata mrithi wa Klopp. Kuja kwa kocha kutoka nje ya Boot Room
maana yake tungeanza upya na Klabu haikutaka hilo. Ndipo msaidizi wa Klopp, Bob
Paisley akachukua timu.
Tunavyozungumza,
Paisley ndo the most decorated manager in Liverpool history. Na ndio kocha wa
kwanza kushinda mataji matatu ya Ulaya. Weka nukta hapo!
Turudi hapa:
Nikaandika pia ni kana kwamba Klopp nae alianzisha new day boot room. Na hapa
ndipo nataka tujadili kwanini namuona Lijnders kama Bob Paisley mpya.
Katika miaka
nane hii ya Klopp, miaka hii mitatu ni kama alianza kumuandaa Lijnders kuchukua
nafasi yake. Alianza kumpa power kubwa ndani ya Timu.
Mosi alimpa
role ya FA na Carabao. Lijnders ndie alikua anaenda kwenye press zote za
mashindano haya. Na hata vikosi akawa anapanga yeye.Jambo ambalo huwezi kuliona
kwa timu nyingine.
Pili Klopp
akampa nafasi kubwa ya kupendekeza wachezaji wa kusajiliwa na Klabu. Darwin
Nunez, Luis Diaz, Diogo Jota, Cody Gapko na Fabio Carvalho zilikua signings za
Lijnders.
Sidhani kama
kuna kocha msaidizi wa timu zingine mwenye nafasi kama hii. Kwahiyo
nashawishika kusema kwamba Klopp alimuandaa Lijnders kumrithi. Tunahitaji kocha
wa kuendeleza project.
Ameandika
James anapenda kujiita Billy Shankly
0 Comments