MISRI WACHEZESHWA
‘NDOMBOLO’ NA CONGO.
CHAMA cha
Soka cha Misri kimefichua kwamba kimechinja ng’ombe kama kafara kwa ajili ya
timu yake kufanya vizuri kwenye fainali za Afcon 2023 zinazoendelea huko Ivory
Coast.
Msemaji wa
chama hicho, Mohamed Morad alisema juzi Ijumaa kwamba ng’ombe amechinjwa na
nyama yake imegawawia kwa watu wenye uhitaji huko Cairo ili kuleta bahati
kwenye timu hiyo.
Misri bado
haijashinda mchezo wowote kwenye fainali za Afcon 2023 na jana Jumapili
ilishuka dimbani kukipiga na DR Congo katika mchezo wa hatua ya 16 bora huko
San Pedro. Timu hiyo ilitoka mji wa Abidjan hadi San Pedro kwa ajili ya mchezo
huo ambao hata hivyo walifungwa kwa penalti
Kambi ya
timu ya taifa ya Misri imekumbwa na majeruhi wengi. Imempoteza supastaa wake,
Mohamed Salah kwa maumivu ya misuli na kipa Mohamed El Shenawy, aliyeumia bega
katika mchezo wao wa tatu.
Emam Ashour
Jumatano aliwahishwa hospitali baada ya kuumia kichwani mazoezini, lakini sasa
amerejea na kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya mikikimikiki hiyo ya hatua ya
mtoano.
Wachezaji wa
Misri waliripotiwa kutoa kafara ya mnyama mazoezini kwao kabla ya kushinda
ubingwa wa Afcon 2008 katika fainali zilizofanyika Ghana.
Misri 1-1 DR
Congo (P 7-8 )
Mostafa
Mohamed 45’
Meschack
Elia 37’
MATUTA
MISRI ✅❌✅✅✅✅✅✅❌
DRC ✅❌✅✅✅✅✅✅✅
DR Congo
itachuana na Guinea katika hatua ya robo fainali.
0 Comments