Mamlaka ya
Israeli imeendelea kuzuia misaada ya kuokoa maisha kufikia kaskazini mwa Gaza
siku 102 tangu mashambulio ya ugaidi yaliyoongozwa na Hamas yaliposababisha
vita, umesisitiza Umoja wa Mataifa akiwemo Katibu Mkuu António Guterres ambaye
ameonya kwamba "Jinamizi la muda mrefu la njaa linawazogoma watu wa Gaza.”
Mafuta, dawa
vimekataliwa kuingia
Katika
taarifa yake ya hivi karibuni juu ya vita ambayo iliyotolewa Jumapili jioni,
OCHA ilibainisha kuwa makao vitu vingi vilivyokataliwa na Israeli vinahusisha
mafuta na dawa zilizotengwa kwa hifadhi, visima vya maji na vituo vya afya
kaskazini mwa Wadi Gaza.
"Ukosefu
wa mafuta kwa ajili ya kusukuma maji, usafi wa mazingira na usafi huongeza
hatari za kiafya na hatari za mazingira. Ukosefu wa dawa umedhoofisha utendaji
wa hospitali sita zinazofanya kazi kwa kiasi kidogo limesema shirika la OCHA na
kuonyesha kuwa " Mashambulizi makali ya Israeli, angani, ardhi na
baharini, kupmbana na na vikundi vyenye silaha vya Palestina yameendelea
kughubika sehemu kubwa ya Gaza, huku makombora yanayovurumishwa na vikundi
vyenye silaha vya Palestina kuingia Israeli
yakiendelea pia”.
Wakati huo
huo, shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeripoti kwamba kituo cha afya
cha Nasser Medical Complex katika mji wa kusini wa Khan Younis
"kinaendelea kupata idadi kubwa ya wagonjwa wenye kiwewe na visa vya
kuungua".
Mzigo mkubwa
kupindukia
Kwa muji wa
WHO hospitali hiyo ina wagonjwa 700 idadi ambayo ni mara mbili ya uwezo wake wa
kawaida wakati kitengo cha ICU na
majeraha ya moto "hakina wafanyikazi wa kutosha na hivyo
kuchelewesha matibabu ya kuokoa maisha".
Maendeleo
hayo yamefuatoa ombo la kusitisha mapigano kwa pande zote lililotolewa Jumatatu
na mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres.
Pia alitaka
kuachiliwa mara moja na bila masharti ya mateka wote waliochukuliwa wakati wa
shambulio la kigaidi la Oktoba 7 na uchunguzi kamili wa madai yote ya
unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanamgambo wa Palestina ufanyike.
"Hatuwezi
kutoa misaada ya kibinadamu wakati Gaza iko chini ya milipuko mizito ya mabomu,
iliyosambaa na isiyo na mwisho," Bwana Guterres alisema, huku alionyesha
wasiwasi mkubwa juu ya uharibifu wa jumla na viwango vya majeruhi kwa raia
ambacho si cha kawaida kwa kipindi chapote ambacho amekuwa Katibu Mkuu.
Guterres
aliendelea kusema kwamba "Wakati kumekuwa na hatua kadhaa zilizopigwa
katika kuongeza mtiririko wa msaada wa kibinadamu ndani ya Gaza, lakini bado
kiasi cha misaada ya kuokoa maisha haijawafikia watu ambao wamevumilia miezi ya
kushambuliwa katika kiwango kinachopaswa na kinachohitajika."
Hivyo
amesema halii inasababisha "Kivuli cha muda mrefu cha njaa kuwaghubika
watu wa Gaza sanjari na magonjwa, utapiamlo na vitisho vingine vya
kiafya."
0 Comments