TIMU ya Singida
Fountain Gate inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara inaendelea na maadalizi
kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu 2023/2024.
Singida Fountain Gate
iliweka kambi Arusha ilirejea Singida kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya tamasha
la Singida Big Day.
Tamasha la Singida Big
Day lilifanyika Agosti 2 2023 na walitambulisha wachezaji wapya na wale
waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2022/23.
Ofisa Habari wa Singida
Fountain Gate, Hussein Masanza amesema: “Timu yetu inajiandaa vyema na msimu
ujao tukiwa na mikakati mizuri.
“Hakuna majeruhi kwa
sasa wachezaji wanaendelea vizuri na mazoezi tunaomba mashabiki watuunge mkono
katika mashindano ninaimani tutafanya vizuri katika mashindano ya ligi.
“Mpago mkubwa ni
kufanya vizuri kwenye mashindano ambayo tunashiriki. Wachezaji wapo tayari na
tunaamini itakuwa hivyo licha ya ushindani kuwa mgumu tupo tayari,”.
Timu hiyo inashiriki
Kombe la Shirikisho Afrika ina kibarua cha kucheza Ngao ya Jamii ikianza hatua
ya nusu fainali dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Agosti 5 Singida
Fountain Gate waliwasili Tanga kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya Ngao ya
Jamii.
Miongoni mwa wachezaji
waliopo kambini ni pamoja na Beno Kakolanya, Meddie Kagere, Joash Onyango.
0 Comments