LEO Agosti 7 Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB) kupitia Afisa Mtendaji Mkuu, Almasi Kasongo, imetangaza ratiba
ya msimu mpya wa 2023/24.
Katika ratiba hiyo inayotarajiwa
kuanza Agosti 15 2023 mchezo wa kwanza wa kufungua pazia utachezwa Uwanja wa
Highland Estate, Mbeya.
Ihefu wao watakuwa nyumbani
wakiikaribisha Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco.
Kasongo amesema mechi ya watani wa
jadi kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC itapigwa Novemba 5, 2023 saa 11:00
jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Katika mechi za mzunguko wa kwanza
kwenye msimu mpya wa NBC Premier League 2023/24, Simba mchezo wake wa kwanza
itakuwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezo wa Simba inayonolewa na Kocha
Mkuu Roberto Oliveira unatarajiwa kuchezwa Agosti 17,2023 Uwanja wa Manungu,
Morogoro.
Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel
Gamondi itaanza nyumbani dhidi ya KMC katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Burudani ya kwanza kwa Yanga
inatarajiwa kuchezwa Agosti 23,2023 ambapo timu hizo zitakuwa kusaka pointi
tatu muhimu.
Ipo wazi kuwa mabingwa watetezi wa
ligi ni Yanga waliotwaa ubingwa huo chini ya Nasreddine Nabi.
0 Comments