NYOTA MPYA YANGA AJA NA UJUMBE HUU
HAFIZ Konkoni mshambuliaji mpya wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kwa
ajili ya msimu mpya wa 2023/24.
Nyota huyo anatajwa kuwa mbadala wa mshambuliaji Fiston Mayele ambaye
amesepa Yanga na kuelekea kupata changamoto mpya ndani ya Pyramids ya Misri.
Mayele ameweka wazi kuwa anaamini wachezaji wapya ambao wapo ndani ya
kikosi cha Yanga pamoja na wale ambao walikuwa pamoja msimu wa 2022/23
watafanya vizuri.
Mshambuliaji huyo mpya raia wa Ghana amesema: “Natambua ushindani ni
mkubwa lakini tutashirikiana na wachezaji wengine kupata matokeo tupo tayari.
Kikubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo tunacheza na
tunaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja
nasi,”.
Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC,
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Agosti 9.
Ikumbukwe kwamba ni timu nne zinashiriki msimu huu ikiwa ni Yanga
yenyewe ambao walitwaa taji hilo msimu wa 2022/23 mbele ya Simba ambao nao
wanashiriki pia, Singida Fountain Gate na Azam FC.
0 Comments