Wakazi wa kijiji cha Kambiri nchini
Kenya wameachwa vinywa wazi baada ya mti uliokatwa na kuanguka chini kupatikana
umesimama tena imara.
Kwa mujibu wa ripoti ya K24 Digital,
wakazi wanasema mti huo uliangamizwa miaka miwili iliyopita lakini sasa
umeibuka tena shambani.
Ni kisa ambacho kimegeuka kuwa fumbo
na sasa wakazi wamekuwa wakifika eneo tukio kushuhudia maajabu hayo.
Kevin Mbalilwa aliambia ripota kuwa
mti huo uliangushwa na upepo mkali miaka miwili iliyopita na hata kuvunjwa
kuni.
Hata hivyo, katika hali ambayo bado
haijaeleweka, mti huo sasa umesimama imara shambani na wakazi hawaamini macho
yao.
Mwenye shamba hilo amewataka maafisa wa Wizara
ya Misitu kufika eneo hilo angalau kujaribu kutatua hali.
"Ninataka maafisa wa mambo ya misitu
kufika hapa ili waniambie vile ninaweza kunufaika na kisa hiki. Watu wamekuwa
wakifika eneo hili kuona kisa hiki na hawanipatii lolote ila kuharibu mahindi
yangu," alisema.
Mkulima huyo anataka sasa mti huo
kugeuzwa na kuwa kivutio kwa watalii akisema shamba lake linapokea wageni kila
siku kuona maajabu hayo.
"Ninaomba maafisa wa KFS wakuje
na wafanye huu mti kuwa kivutio cha watalii ili nipate kitu," alisema kwa
wanahabari.
Baadhi ya wakazi hata hivyo wanasema
hawawezi kufika eneo hilo kamwe wakihofia kuwa huenda kilichotokea ni mwiko.
Wanasema ni lazima familia husika kuita wazee ili matambiko yanayofaa yafanywe
na kugeuza hali.
0 Comments