Muigizaji wa
filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amefunguka na
kudai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameletwa duniani na Mungu kwa
lengo la kusaidia watu nasio vinginevyo.
Wema ametoa
kauli hiyo mara baada ya Mhe. Makonda kuonesha nia ya kumsaidia kumsafirisha
kijana Ahmed Albaity kwenda nchini China kwa lengo la kupatiwa matibabu juu ya
ugonjwa aliokuwa nao wa kupooza mwili mzima.
"Nikisema
'RC' wangu ni mtumishi wa Mungu basi namaanisha, mimi 'sometimes' nasema
uliletwa duniani kuja kufanya ya Mola wako tu. Mungu azidi kukubariki 'my RC
you are just like a guardian angel', ipo siku wataelewa tu. 'I got a Good
Feeling about Ahmed and Inshallah God will work a miracle, kila lenye mwanzo
halikosi kuwa na mwisho", amesema Wema Sepetu.
Kijana Ahmed
Albaity alipooza mwili wake mnamo 2007 baada ya kucheza vibaya michezo ya
kujirusha 'dive' katika bahari na kwa bahati mbaya alikosea na kujipiga kichwa
chini ambapo ilipelekea kupata matatizo yote hayo mpaka sasa.
0 Comments