Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa onyo kali kwa kampuni zinazofanya kazi ya
kukamata pikipiki (bodaboda) kwa mtindo wa kuvamia kitendo kinachohatarisha
usalama wa dereva na abiria.
Makonda
amesema zipo baadhi ya kampuni zimekuwa zikivizia madereva wa bodaboda kisha
kuwavamia na kuwakamata na wakati huohuo kuwapiga kitendo ambacho amesema
hawezi kukiruhusu kiendelee kwenye mkoa wake.
Makonda
ametoa onyo hilo wakati wa kikao na madalali wanaotekeleza hukumu za mahakama
na benki kilicholenga kuwatambua na kupitia nyaraka zinazowapa mamlaka ya
kufanya kazi hiyo ili wasionekane matapeli na waweze kupata ushirikiano wa
serikali.
Uamuzi wa
Makonda kukutana na madalali hao ni manyanyaso na ukandamizaji unaofanywa na
baadhi ya madalali wanaopiga minada nyumba, magari, viwanja, mashamba, ofisi na
mali za watu bila kufuata taratibu na kusababisha maumivu makali kwa wananchi.
Amesema zipo
kampuni za udalali zinazofoji nakala za hukumu, mihuri, sahihi za mahakama,
ofisi ya Mkoa, wilaya na mitaa na wakati mwingine kufanya minada bila kufuata
taratibu.
Kutokana na
hilo Makonda amezitaka kampuni zote za udalali Dar es salaam kuwasilisha nakala
za nyaraka ya usajili kwa mwanasheria wa mkoa zipitiwe na kujiridhisha ili
wapewe ushirikiano na serikali.
Nao madalali
wamemshukuru Makonda kwa uamuzi wa kuwatambua ili wapate ushirikiano wa
serikali kwakuwa wapo baadhi ya madalali waliokuwa wakifanya kazi hiyo kinyume
na sheria na kuwachafulia kazi wale wenaofata taratibu za kazi hiyo.
0 Comments