Msichana
mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata ya Kipindu wilayani
Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na polisi akituhumiwa
kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.
Wananchi
wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo
wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha
na vipande vya khanga na kumuweka kwenye kikapu alichokificha chini ya uvungu
wa kitanda chake.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini
Namanyere.
Kamanda
Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilaya Nkasi na kwamba
atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio kukamilika. Wakizungumza
baadhi ya wanawake wamedai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi
lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake.
0 Comments