Mahakama ya
Wilaya ya Dodoma imemuamuru mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka katika taasisi
ya magonjwa ya akili mshtakiwa Onesmo Machibya maarufu Nabii Tito, ili kujua
iwapo ana akili timamu au la.
Hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama hiyo, James Karayemaha ametoa agizo hilo leo Jumatatu
Februari 19,2018.
Amesema
Magereza wanachelewesha haki ya mshtakiwa na kwamba, anashangaa ni kwa nini
wanashindwa kutekeleza agizo la kumpeleka kufanyiwa uchunguzi.
"Naagiza
amri ya Mahakama itekelezwe, apelekwe taasisi ya magonjwa ya akili Isanga
(Mirembe) si kama alivyoleta vielelezo kutoka Muhimbili," amesema
Karayemaha.
Hakimu
ameahirisha kesi hadi Machi 5,2018 itakapotajwa kwa ajili ya kupokea taarifa ya
uchunguzi.
0 Comments