MAHAKAMA ya
Wilaya ya Dodoma imeagiza mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma Tito
Machibya, maarufu kama ‘Nabii Tito’ (45) kupimwa akili upya katika Taasisi ya
Afya ya Akili ya Mirembe Isanga mkoani Dodoma ili kujiridhisha kama ana
matatizo ya akili.
Licha ya
kuagizwa mtuhumiwa huyo kufanyiwa vipimo upya, mahakama pia imetaka
kuwasilishwa kwa vielelezo kama kweli ana tatizo hilo kama alivyoieleza
mahakama.
Nabii Tito
anashtakiwa kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kutumia wembe.
Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, alisema jana kuwa kutokana na
mshtakiwa kuieleza mahakama kuwa ana matatizo ya akili na alifanya tukio hilo
kutokana na kusikia vitu ambavyo vilikuwa vinamwamuru akate, mahakama itabidi
ipate vielelezo ambavyo vitathibitisha anachokisema.
Karayemaha
alisema kutokana na kifungu namba 219 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya
Jinai, kama mshtakiwa atabainika kweli ana matatizo ya afya ya akili, mahakama
itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili timamu, hivyo hana hatia.
“Mshitakiwa
anadai kuwa ana matatizo ya akili na amekuwa akitibiwa katika hospitali
mbalimbli ikiwemo ya Maweni. Mahakama hii inaagiza vielelezo vyake vyote
viletwe hapa lakini pia apelekwe kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili
Mirembe Isanga,” alisema Karayemaha.
Pia alisema
kama mshtakiwa atabainika kuwa hana tatizo lolote la afya ya akili kwa mujibu
wa vielelezo vyake pamoja na vipimo atakavyofanyiwa, atakuwa na kesi ya kujibu.
“Kutokana na
hili aliloiambia mahakama kuwa ana matatizo ya akili hata suala la dhamana
tunaliweka pembeni kwanza kwa sababu hawezi kujieleza lakini kama itabainika
kuwa hana matatizo ya akili kutokana na vielelezo vitakavyoletwa pamoja na
vipimo vitakavyofanyika, suala la dhamana litafanyiwa kazi,"alisema.
Hata hivyo
alisema mshtakiwa huyo anarudi rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa Februari 19,
mwaka huu.
Wakati kesi
itakapotajwa vielelezo vyote pamoja na vipimo vinatakiwa kuwa tayari
vimeshawasilishwa mbele ya mahakama hiyo.
Nabii Tito
anashtakiwa kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa kujikata
0 Comments