Wimbo wa
'Subalkheri Mpenzi', ulioimbwa na wasanii wa kizazi kipya Aslay Ishack na
Nandy, umezidi kuzua utata baada ya mmiliki wa wimbo huo, Kikundi cha Tarab
Asilia visiwani Zanzibar (Culture Music Club), .........Kudai kuwa watawaburuza
mahakamani kwa kuwa Sh. 800,000 zilizotolewa kama fidia hawazitambui.
Katibu
Mtendaji wa kikundi hicho, Taimur Rukuni Twaha, jana alisema wasanii hao kabla
ya kuimba tena upya wimbo huo walipaswa kuonana na uongozi huo ili kukubaliana
jambo ambalo hawakufanya hivyo.
Kwa mujibu
wa katibu huyo, wasanii wa kikundi hicho waliopewa mgawo huo wa fedha ni
waimbaji wawili (majina tunayo) ambao mmoja alipewa Sh. 500,000 na mwingine Sh.
300,000.
“Walichokifanya
Aslay na Nandy kwenda kwa waimbaji wetu na kuwapa kiwango hicho cha fedha kwetu
tunaona hakikubaliki na wametoa kama zawadi tu kwa sababu thamani ya wimbo wetu
haulingani na kiwango hicho,” alisema Twaha.
Alisema kwa
mujibu wa katiba ya kikundi hicho, ibara ya sita inaeleza nyimbo zote
zilizoimbwa na kikundi ni mali ya kikundi na kwamba muimbaji, mtunzi na muweka
sauti watakuwa na haki zao kupitia kikundi hicho.
Alisema
kimsingi msimamo wao utabaki pale pale wa kuwafikisha mahakamani wasanii hao
endapo watashindwa kutimiza masharti waliopewa na uongozi wa kikundi hicho.
Aidha,
alisema masharti hayo hayatomhusu Aslay na Nandy peke yao bali na mwanamuziki
Hussein Mmanga Faki (maarufu HamaQ) na mwenzake Mosi Suleiman kwa kuimba wimbo
wa 'Mke wa Awali ni Wewe Aziza' ambao pia ni mali ya kikundi hicho.
“Tunafahamu
kuwa nyimbo zetu wameziimba tena kwa lengo la kibiashara na wamekuwa wakipata
fedha kupitia nyimbo hizo,”alisisitiza katibu huyo.
Alisema
tayari wameshawaandaa mawakili wao, ambao wataisimamia kesi hiyo mahakamani
iwapo wasanii hao watashindwa kutimiza masharti waliyopewa.
Akizungumzia
suala hilo, Meneja wa Coconut FM, ambaye ni mwakilishi wa Aslay na Nandy,
alisema kuwa wasanii hao watafikishwa katika uongozi wa Kikundi cha Taarab
Asilia (Culture) ili kupata suluhu.
Alisema wao
hawana makosa kutumia wimbo huo, kwani kabla ya kurudia kuuimba walishakutana
na mtunzi wa wimbo huo Bakari Abeid ambaye sasa ni marehemu na kumalizana naye
wakati wa uhai wake.
0 Comments