
Ni rahisi
sana kwa shabiki kindakindaki wa mpira wa miguu kuwa mchawi katika maisha
halisi kuliko shabiki kindaki ndaki wa muziki.
Hii ni kwa
sababu shabiki wa timu moja ya mpira wa miguu hawezi kuwa shabiki wa timu
nyingine ya mpira wa miguu ambayo inashiriki katika ligi moja na timu yake .
Kwa mfano
Shabiki wa Yanga hawezi kuwa shabiki wa Simba wala kufurahishwa na mafanikio ya
Simba kama ambavyo Shabiki wa Simba hawezi kuwa shabiki wa Yanga wala
kufurahishwa na mafanikio ya Yanga.
Shabiki wa
Real Madrid hawezi kuwa shabiki wa Barcelona wala kufurahishwa na mafanikio ya
Barcelona na kinyume chake.
Ili hali
katika upenzi wa muziki hali ni tofauti sana. Shabiki wa Msondo Ngoma ana weza
kupendezwa na nyimbo za wana Sikinde Ngoma ya Ukae kama ambavyo shabiki
kindakindaki wa wana Sikinginde Ngoma ya Ukae anavyo weza kufurahishwa na
nyimbo za Msondo Ngoma.
Shabiki
kindaki ndaki wa Diamond Platnumz anaweza kuwa mpenzi mkubwa sana wa nyimbo za
Ali Kiba kama ambavyo Shabiki wa damu wa Ali Kiba anavyo weza kuwa mpenzi
mkubwa wa nyimbo za Diamond Platnumz.
Shabiki
kindakindaki wa Davido anaweza kuwa mpenzi wa kutupwa wa nyimbo za Wizkid kama
ambavyo shabiki wa kutupwa wa Wizkid anavyo weza kuwa mpenzi mkubwa wa nyimbo
za Davido.
Shabiki
kindaki ndaki w a AKA anaweza kuwa mpenzi wa kutupa wa nyimbo za Casper Nyovest
kama ambavyo shabiki wa damu wa Casper Nyovest anavyoweza kuwa mpenzi mkubwa wa
nyimbo za AKA.
Shabiki
kindakindaki wa Tupac Shakur anaweza kuwa mpenzi wa damu wa nyimbo za Notorious
BIG kama ambavyo shabiki kindakindaki wa Notorious BIG anavyo weza kuwa mpenzi
wa damu w a nyimbo za Tupac Shakur.
Lakini hali
ni tofauti sana kwa mashabiki wa mpira wa miguu. Ushabiki wa mpira wa miguu
unapo tamalaki unaweza kunmfanya shabiki husika akawa na tabia ama hulka ambazo
hazina tofauti na hulka za wachawi.
Kitendo cha
shabiki wa timu moja kutofurahishwa na mafanikio ya timu nyingine ambayo haya
iathiri timu yake hakina tofauti yoyote na mchawi ama mshirikina ambae
anaumizwa kwa sababu mtoto wa jirani yake amefaulu na kuchaguliwa kujiunga na
chuo kikuu.
Mfano mzuri
ninao kwa shabiki mmoja wa mpira wa miguu ambae jina na mahali anapotoka nina
muhifadhi.
Shabiki huyu
alinipigia simu yangu juzi na kunieleza kwa uchungu mkubwa sana kuwa yeye ni
shabiki wa kufa wa klabu ya Arsenal na kwamba ameumizwa sana na kitendo cha
mchezaji Sanchez kuuzwa kwenda Manchester United.
Shabiki huyo
akaendelea kunieleza kama ifuatavyo :
"NATAKA
UMFUNGE SANCHEZ. FUNGA MIGUU YAKE, AKIENDA MAN U ASIFUNGE HATA GOLI MOJA. FUNGA
AKILI YAKE AKIWA UWANJANI ASAHAU KAMA YUPO UWANJANI . FUNGA KUMBUKUMBU ZAKE
AKIFIKA GOLINI ASAHAU GOLI LILIPO. MTIE MALIENGE KWENYE MACHO YAKE AKIWA NA
MPIRA AWE ANAONA GOLI LIKO PEMBENI APIGE PEMBENI NA KUKOSA GOLI. GOLI PEKEE
AMBALO ATATAKIWA KUFUNGA LIWE GOLI LA KUJIFUNGA MWENYEWE NA SI VINGINEVYO.
MFARAKANISHE
NA WACHEZAJI WENZAKE, KOCHA WAKE NA MASHABIKI WAKE. NA MWISHO WA SIKU ATUPIWE
VIRAGO NA KUONDOKA KWA AIBU.. MFICHE UWANJANI ASIONEKANE UWANJANI. AU MTIE
MAJERUHI , AUMIE KWENYE MAZOEZI KABLA YA KUANZA KUITUMIKIA KLABU YAKE AKAE
AKIWA MAJERUHI KWA MSIMU MZIMA NA TIMU YAKE IMCHOKE NA KUMTUPIA VIRAGO
..ASIONEKANE UWANJANI NA KAMA IKITOKEA BAHATI MBAYA AMEONEKANA UWANJANI BASI
AONEKANE AKIWA AMEKAA KWENYE BENCHI NA IKITOKEA AKICHEZA MECHI BASI TIMU YAKE
IFUNGWE MAGOLI MENGI NA AWE NI MTU WA KUKOSA MAGOLI MARA ZOTE… NIPO TAYARI KWA
LOLOTE DOKTA . NINAKUOMBA SANA DOKTA UNISAIDIE KWA HILO”
Shabiki huyu
aliongea mambo mengi sana kwa uchungu mkubwa sana.
Maneno ya
shabiki huyu wa mpira wa miguu yalinirudisha miaka sita nyuma. Nikakumbuka
mwaka 2012 Robin Van Persie alivyo hamia Man U kutoka Arsenal, mashabiki wengi
sana wa Arsenal hawakufurahishwa na mmoja kati ya mashabiki hao alinitafuta na
kuniambia :
“ DOKTA. ,
MIMI NI SHABIKI MKUBWA SANA WA ARSENAL. MIMI NI MFANYAKAZI,. OFISINI KWETU KUNA
WAFANYAKAZI WENZETU WAWILI MASHABIKI WA MAN U AMBAO WANA DHARAU SANA NA MANENO
YA KEJELI SANA HASA TIMU YANGU YA ARSENAL INAPOKUWA IMEFUNGWA. MIMI NINAOMBA
UFANYE DAWA ZAKO HAWA JAMAA WAFUKUZWE KAZI AU WAHAMISHIWE KWENYE MIKOA YA MBALI
KABISA. ILI NISIWAONE WAKIWA WANAFURAHIA MAGOLI YANAYO FUNGWA NA VAN PERSIE
AKIWA AMEVAA JEZI YA MAN U.
NINAJUA VAN
PERSIE NI MCHEZAJI HATARI SANA NA SITAKUWA TAYARI HATA KIDOGO KUWAONA FULANI NA
FULANI ( ANATAJA MAJINA YAO ) WAKIWA WANAFURAHIA USHINDI W A TIMU YAO KWA
MAGOLI YALIYO FUNGWA NA VAN PERSIE. NITAUMIA SANA “
Kwa Mifano
hiyo miwili unaweza kuona mahali ambapo ushabiki wa mpira wa miguu una weza
kukufikisha.
Katika
ulimwengu wa michezo ni jambo la kawaida sana kwa shabiki wa timu Fulani
kutofurahi pindi timu yake inapo fungwa au kupata matokeo mabaya . SIna tatizo
katika hili.
Ninacho
kisema hapa ni pale wewe shabiki wa mpira wa miguu unapofikia hatua ya
kuichukia timu pinzani kiasi cha kutofurahishwa na mafanikio ya timu hiyo
pinzani hata kama haya kuathiri au kuiathiri timu yako kwa chochote.
Hiyo ndio
tunayo ita roho ya kichawi na uchawi.
Mfano mzuri
ni huu hapa. Wewe ni shabiki wa Arsenal, timu yako imefuzu kuingia NNe bora na
umesha maliza mechi zako zote. Wapinzani wako Man U wamebakiza mechi moja tu na
wanatakiwa wapate pointi tatu ili nao waweze kufuzu kuingia nne bora. Bahati
nzuri Man U wanashinda na kuingia nne bora. Wewe shabiki wa Arsenal unachukia
na kukasirika kabisa kwa sababu Man U na wao wamefuzu kuingia nne bora.
Unapofikia katika hatua hii ndipo unapokuwa katika levo moja na wachawi kwa
sababu wachawi pia hawapendi kuuona mafanikio ya watu wengine hata kama hayawa
athiri kwa chochote..
Ukitafakari
suala hili kwa jicho la tatu utagundua kuwa chuki uliyo nayo dhidi ya mafanikio
ya timu pinzani mara nyingi huwa ni chuki dhidi ndugu, jamaa, na marafiki zako.
Hii ni kwasababu ifuatayo :
“ MARA ZOTE
SHABIKI WA TIMU FULANI ANAPO CHUKIZWA NA MAFANIKIO YA TIMU PINZANI HUWA ANAKUWA
HACHUKIZWI NA MAFANIKIO YA WACHEZAJI AU TIMU HIYO PINZANI BALI HUWA ANACHUKIA
KUONA JIRANI, JAMAA, AU NDUGU NA MARAFIKI ZAKE AMBAO NI MASHABIKI WA TIMU HIYO
PINZANI WAKIWA WANAFURAHIA MAFANIKIO YA TIMU HIYO PINZANI NA SI VINGINEVYO “
Kwa hiyo
chuki yako wewe sio chuki dhidi ya timu pinzani, ila ni chuki dhidi ya jirani
yako unaeonana nae kila siku ambae ni shabiki wa timu pinzani. Hutaki kumuona
akiwa anafurahia na unafurahia kumuona akiwa anahuzunika pindi timu yake
pinzani inapo pata matokeo mabaya.
Roho au
hulka hiyo haina tofauti na roho ya kichawi. Mfano, mwanzoni mwa miaka ya
tisini kuna kijana mmoja kutoka mkoa mmoja wa hapa hapa Tanzania, baada ya
kuhitimu masomo yake, alipangiwa kufanya kazi kwenye tarafa moja iliyopo katika
mkoa mwingine hapahapa nchini.
Tarafa hiyo
inasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya magwiji wa uchawi na ushirikina na ipo
tofauti kabisa na kata nyingine zote zilizopo katika mji huo ambao ni miongoni
mwa miji yenye maendeleo makubwa hapa nchini.
Wazazi wa
kijana huyo walimuhasa atakapo fika katika tarafa hiyo, awe na nidhamu na
heshima ya hali ya juu sana. Awaheshimu watu wote bila kujali hali zao kimaisha
au umri
wao na
kikubwa zaidi, awaheshimu sana wazee.
Huyo kijana
baada ya kupangiwa kazi kwenye tarafa hiyo, wazazi wake walimuhasa akifika
katika tarafa hiyo awaheshimu watu wote, wakubwa kwa wadogo, asiwe na dharau na
kikubwa zaidi awe na ukaribu sana na wazee.
Hao wazee
ndio watakuwa baba zake ambao watamlinda na kumuongoza na kumfanya aishi salama
katika tarafa hiyo. ( KATIKA TARAFA HIYO WAZEE WANAHESHIMIKA SANA NA HUWA
HAWAITWI “BABU” BALI BABA )
Kijana
alipofika katika tarafa hiyo akaanza kufuata maelekezo aliyo elekezwa na
wazazi. Alikuwa na heshima ya hali ya juu sana. Ndani ya muda mfupi tu akawa
ameshajulikana kwa magwiji wa tarafa hiyo. Kijana alikuwa akipata mshahara
wake, atanunua sukari, chumvi, mchele , sabuni na vitu vingine na kuwagawia
magwiji wa tarafa hiyo. Nadhani alikuwa muumini wa methali isemayo “ Mchawi mpe
mwana akulelee “, isipokuwa tu yeye aliamua kujikabidhi yeye mwenyewe wamlee. “
Kila siku
jioni ilikuwa lazima aende kuripoti kwa wazee hao kama ishara ya kuonyesha
heshima, adabu na utiifu kwao. Siku ambayo hakuripoti basi kulikuwa na sababu
isiyo weza kuzuiliwa na binadamu na akionana nao kesho yake lazima awaombe
radhi.
Kijana huyu
alikuwa mjasiriamali pia. Akiwa katika tarafa hiyo akagundua fursa kubwa ya
biashara ya mbao na vifaa vya ujenzi pamoja na udalali wa viwanja na mashamba
kwa sababu mji ulikuwa unapanuka na watu wengi walikuwa wana jenga kwa kasi.
Jamaa
akaenda kuchukua mkopo benki na kuingia kwenye biashara ya mbao ambayo
haikuchelewa kuanza kumlipa.
Kijana akawa
anatengeneza pesa za kutosha na hata matunzo kwa wale ‘magwiji’ yakaongezeka.
Baada ya kipindi
kichache Yule kijana akaanza kuwaambia magwiji hao sentensi ambazo
hawakuzipenda.
Hawakupendezwa
na sentesi hizo kwa sababu zilikuwa na maana mbaya sana katika tafsiri ya
kamusi ya kichawi.
Labda tu kwa
wasio fahamu, wachawi wana kamusi yao. Moja kati ya kazi za kamusi ya kichawi
ni pamoja na kutafsiri maneno, ishara na vitendo mbalimbali vinavyo fanywa na
watu mbalimbali.
Nyuma ya
kila sentensi unayo izungumza, huwa kuna sentesi nyingine ya kichawi. Nyuma ya
kila kitendo unacho weza kukifanya huwa sentensi ya kichawi.
Kwa mfano :
“ A “ ni Kijana mwenye umri wa miaka 25. Kijana huyu amezaliwa na kukulia
kwenye kijiji “ X “. Kijiji hiki ni kijiji ambacho wakazi wake wengi ni wachawi
na washirikina.
Ndani ya
kijiji hiki hakuna maendeleo. Watoto wa kike na kiume kutoka katika kijiji hiki
wote wameharibikiwa na hakuna alietoka katika maisha hata mmoja.
Kwa bahati
nzuri au mbaya huyu kijana “ A “ baba ake alikuwa na mwamko w a elimu,
akampeleka “ A “ kwenye shule za bweni ambako ameweza kusoma kuanzia shule ya
msingi hadi chuo kikuu. Alikuwa anarudi kijijini kimya kimya kusalimia kisha
anarudi mjini kuendelea na masomo yake.
Baada ya
kuhitimu Chuo Kikuu, siku moja “ A “ anaenda kutembelea kijijini kwao. Na kwa
bahati mbaya au nzuri “ A “ anakutana na mzee “ Y “. Huyu ni mzee ambae
anaheshimika na kuogopeka sana hapo kijijini kwa sababu "ugwiji " na
“ A “ anamfahamu fika mzee huyu tangu akingali mdogo.
Kwa sababu
kijana “ A “ amelelewa katika mazingira ya heshima, anapokutana na mzee “ Y “
kijana huyu anamsalimia kwa heshima na adabu zote na kama hiyo haitoshi, A
anamsaidia mzee “ Y “ kubeba mzigo wake , hadi nyumbani kwa mzee “ Y “
Hapo Kijana
“ A “ atafarijika moyoni kwamba nimetengeneza sifa ya kuwa kijana mzuri kwa
adabu na heshima niliyo muonyesha mzee huyu.
" A
" anajiona yupo salama na kwamba ametengeneza urafiki na mzee " Y
" .
Lakini kwa
mzee “ Y “ ambae ni mchawi na mshirikina yeye atakitafisiri kitendo cha kijana
“A “ kwa namna tofauti sana. Akitafsiri kwa kutumia kamusi ya wachawi.
Atakitafsiri
kitendo cha kijana “ A “ kama ifuatavyo :
“ DUH! YANI
HUYU KIJANA WA MZEE “ X “ PAMOJA NA KUWA NA UMRI WA MIAKA 25 LAKINI
AMENIONYESHA HESHIMA NA ADABU YA HALI YA JUU KIASI HIKI?
HAIWEZEKANI
HATA KIDOGO. KIJANA WA MIAKA 25 ANANIONYESHA HESHIMA NA ADABU KUBWA KIASI HIKI.
INA MAANA BADO TU HAJAHARIBIKIWA?!!! INA MAANA HAVUTI BANG1!!! SIO MLEVI WALA
HANA MAKUNDI!!! HAIWEZEKANI !!! SIWEZI KUKUBALI UPUUZI HUU HATA KIDOGO!!!
MIMI AMBAE
SIO BABA AKE WALA SINA UNDUGU NAE AMENIONYESHA ADABU NA HESHIMA KUBWA KIASI
HICHO, WAKATI WATOTO WANGU WA KUZAA MWENYEWE WENYE UMRI SAWA NA WAKE,
WAKIKUTANA NA MIMI WANANIPIGA VIKUMBO, KAMA HIYO HAITOSHI HUWA WANANITUKANA
HADI TUSI LA MAMA NA KIPIGO JUU!!!.INA MAANA HUYU KIJANA” A” BADO HAJA
HARIBIKIWA ? KAMA MIMI TU AMBAE SIO BABA AKE AMENIONYESHA HESHIMA KUBWA NAMNA
HII, VIPI KUHUSU BABA AKE? SI ITAKUWA MARADUFU!!! HAIWEZEKANI HUYU MZEE “ X “
HAWEZI KUFURAHIA HESHIMA YA MTOTO WAKE WAKATI MIMI KILA SIKU NALIA NA UCHUNGU
KWA USHENZI NINAO FANYIWA NA WANGU WA KUWAZAA MWENYEWE !!! LAZIMA NIMROGE HUYU
KIJANA NA LAZIMA NIMRIPOTI KWENYE KIKAO!!!!
Baada ya
hapo Mzee “ Y"atakacho kifanya ni kwenda kumripoti kijana “ A “ kwa mkuu
wa kilinge.( , VILINGE VYA WACHAWI HUWA VIPO KARIBU KATIKA KILA SEHEMU NA MARA
NYINGI HUWA VINAKUWA KWENYE MITI MIKUBWA NA HUWA VINAKUWA MAJINAAMBAYO MARA
NYINGI HUBEBA MAJINA YA MAENEO. MFANO “ Mbuyuni”, “Mwembeni” “Mkuyuni”” Mwembe
….” Nakadhalika.
Kitakacho
tokea baada ya wiki au miezi kadhaa wazazi wa kijana “ A “ wataanza kumuona
kijana wao amebadilika kitabia katika namna ambayo hawakuitegemea wala
kuitarajia.
Kijana msomi
wa chuo kikuu utamsikia anazungumza maneno ya ovyo kama vile “ Oyaa Bi.
Mkubwaa“, au “ Mshua unazingua !!“ na maneno mengine kama hayo pamoja na
kufanya vitendo vya kilofa kama kuvalia suruali chini ya makalio, kunyoa
viduku, kunywa viroba,kushinda bar anapiga story na wahuni na mwisho wa siku
hayo ndio yanakuwa maisha yake .
Washirikina
na wachawi huwa wanaishi maisha ya hovyo sana sema tu huwa wanajikaza mambo yao
yasijulikane. Ubaya wanao wafanyia watu wengine huwa unawarudiaga wao wenyewe
saba mara sabini hata baada ya miaka mingi.
Mchawi
anapokufanyia ubaya huwa ni kama anajiwekea mwenyewe akiba ya ubaya ambao
utakuja kumtokea baadae kabla ya muda wake wa kuishi haujamalizika hapa
duniani. Kwa hiyo usishangae mzee Y anapo kasirika kusalimiwa kwa heshima na
adabu na kijana A .
Katika
uhalisia hayo ndio maisha ya wachawi katika levo ya familia. Kuna kisa kimoja
kilitokea mwishoni mwa miaka ya themanini katika tarafa hiyo hiyo niliyo itaja
hapo juu. Alihamia mtendaji mpya wa mtaa kutoka mkoa mwingine, baada ya kama
wiki mbili hivi ikaletwa kesi ofisini kwake,. Kuna mzee mmoja gwiji amepigwa
kwa mabapa ya mapanga na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe alieitwa Kulwa . Mzee
alishachukua PF3 tayari na kwenda kutibiwa polisi, jalada lilishafunguliwa
kituoni na huyo Kulwa yupo ndani . Sasa mzee gwiji ameingiwa na huruma ya uzazi
anataka kwenda kumdhamini mahakamani mtoto wake japo yeye ndio muhanga wa tukio
la uhalifu lililo fanywa na mwanae. Kwa kuwa mzee alikuwa anajisikia vibaya
hawezi kwenda ofisini kwa mtendaji kuchukua karatasi ya dhamana, akamtuma
shemeji yake, yaani mdogo wa kiume wa mke wake.
Shemeji mtu
alipofika kwa mtendaji na kumsimulia kilicho tokea, mtendaji alisikitishwa
sana.. “ Alihoji inakuwaje mtoto unampiga kwa mapanga baba ako mzazi! Dunia
imekwisha “ . Wakati mtendaji ana saini karatasi za dhamana, akawa ana mdadisi
yule shemeji mtu “ Imekuwaje kuwaje mpaka huyo kijana akampiga mapanga baba ake
mzazi ?”.. Shemeji mtu akajibu “ Bwana we mambo ya kifamilia ndugu yangu !|.
Mtendaji akasema “ Mambo ya kifamilia?!! Yani mambo ya kifamilia ndio mtu
ampige mapanga baba ake mzazi ?!! DU sijawahi kusikia hiyo ndio naisikia mara
ya kwanza”. “ Ila vyovyote vile, tuchukulie kwamba kweli huyo kijana aliudhiwa
na baba ake kiasi cha kuamua kumshambulia kama njia ya kumaliza hasira zake.
Kwanini basi asinge mpiga u hata ngumi, kwa sababu hayo mapanga si angeweza
kumuua kabisa!! Na angemuua tungekuwa tunaongea habari nyingine tena “
Shemeji mtu
akajibu “ Kulwa ampige ngumi baba ake ? Kulwa hanaga muda wa kurusha ngumi
kumpiga baba ake. Kulwa yeye huwa anampigaga na mapanga tu au silaha yoyote ile
itakayo kuwa karibu nae. Mwenye muda wa kurusha ngumi ni dotto. Dotto ndio huwa
anampigaga ngumi baba ake. Aaaaaah huwa anampiga sana tena sana. Na kizuri baba
mtu mwenyewe analitambua hilo. “ Shemeji mtu akaendelea kusema “ Lakini hata
hivyo pamoja na kwamba Dotto huwa anampiga baba ngumi baba ake mzazi lakini
huwa zinakuwa ngumi kali kweli kweli, unajua Dotto ni mtu wa mazoezi sana na
ana maguvu sana. Mtoto kidogo mwenye afadhali ni kaka yao mkubwa na kina Dotto
yeye huwa anamtia bakora tu baba yao. Yeye hanaga muda wa kushika silaha wala
kumpiga ngumi, yeye huwa ni bakora tu. Na baba mtu anajua, kaka yao mkubwa
akiwepo kama kuna sehemu ya kuchuma fimbo karibu , huwa hafanyi kabisa ujinga
ujinga, kwa sababu anajua kijana wake atamtandika na bakora “
Mtendaji
akataka kujua sababu inayo wafanya vijana hao wawe wanamkosea baba yao mzazi
kwa kumpiga. Shemeji mtu akajibu, huyu mzee huwa anampigaga sana mama yao
akitoka kwenye ulevi halafu akiwaga na hela huwa anaenda kuzimalizia kwa
michepuko huko. Sasa vijana huwa wakisikia mama yao kapigwa au katukanwa, na
wao huwa wanampiga baba yao. Wakimkuta na mchepuko pia huwa wanampa kisago baba
yao.
Yule
mtendaji alilewa na kubaki kusema “ Du ! Yani huyu mzee watoto wake wote huwa
wanampiga . Dunia imekwisha “
Hao Kulwa na
Dotto wakati wanafanya ujinga huo wa kumpiga baba yao walikuwa na miaka 37 na
kaka yao alikuwa na miaka 40.
Katika
mzingira kama hayo mzee kama huyu ambae watoto wake wa kuzaa mwenyewe wanampiga
ngumi, mapanga na fimbo, hawezi kufurahishwa na heshima au adabau kutoka kwa
kijana mtoto wa jirani yake . Huwa wanaumia sana.
Ndio maana
miaka ya nyuma, vijana walishauriwa na kuambiwa kama hawana kinga ya wachawi
wasi jipendekeze kabisa kwa wachawi kama alivyo fanya kijana A. Kuliko
kujipendekeza ni bora wakae nao mbali kabisa. Kuliko kuonyesha wao ni vijana
wenye adabu, bora wajifanye kujitoa akili pindi wanapo kutana na wazee wa aina
hii hususani katika maeneo kama vile misibani nakadhalika. Huambiwi uwatukane,
hapana, wewe kaa kimya na kama utalazimika kuzungumza basi zungumza mambo
yanayo onyesha una maisha magumu, huna matumaini na umeharibikiwa kimaisha.
Unatumia hiyo kama njia ya kuwapumbaza watu wabaya.
Jambo
lingine ambalo ni la kawaida sana katika ulimwengu wa nyama lakini lina maana
mbaya sana kwenye kamusi ya wachawi ni “ Sauti ya mtoto mchanga akilia “.
Hakuna jambo lenye maana mbaya katika ulimwengu wa wachawi kama kusikika sauti
ya mtoto mchanga akilia,na mbaya zaidi sauti hiyo itokekwenye nyumba ya eidha
watu wa swala au ibada au ambao wamefunga ndoa halali.
Hakuna jambo
linalo wakera kama kusikia sauti ya mtoto mchanga akilia kutoka katika familia
ambayo mke na mume wameoana kwa ndoa rasmi.
Nirudi tena
kwa kijana wetu.
Kijana huyu
alianza kuwapigia wazee hao stori kama vile “ Nimepata kiwanja sehemu Fulani “.
“ Nimeanza kufyatua matofali “ mara aanze kuwaambia “ Nimetoka kumpeleka fundi
saiti kwangu “ au “ kesho nitaenda mjini kuchukua mabati, mbao “ na hadithi
zinazo fanana na hizo.
Kijana huyu
alikuwa anawaeleza wazee hao mipango yake kwa nia njema kabisa.
Aliwachukulia
kama wazazi wake na alikuwa akiwaambia hivyo ili labda wampe ushauri wa kufuata
hususani katika suala zima la “ ulinzi wa kiroho “
Ambacho
hakukijua kijana huyo ni kwamba, sentensi alizo kuwa anazitamka kwa wazee hao,
zilikuwa na maana mbaya sana katika kamusi ya uchawi.
“ Sisi
tunaishi kwenye nyumba za udongo. Si watoto wetu wala wajukuu zetu ambao
wamewahi kuwa na nyumba zao wenyewe achilia mbali nyumba ya kisasa kama anayo
taka kuijenga kijana huyu.. Haya ni matusi makubwa sana kwetu.Hatuwezi
kukubaliana na upumbavu kama huu!!! “
Wazee
walicho kifanya wakaamua kumtia nuksi kijana huyo. Kwanza akafukuzwa kazi.
Akashindwa kulipa mkopo benki, nyumba yake aliyokuwa anaijenga ambayo ndio
kwanza ilikuwa imefikia kwenye lenta,ikapigwa mnada ( NYUMBA NYINGI KATIKA
TARAFA HIYO HUWA ZINAISHIA KWENYE LENTA HUKU WAMILIKI WAKISALIA KUWA WALEVI
WAKUPINDUKIA ).
Biashara
yake ikafa. Akaingia kwenye ulevi wa pombe ulio pindukia.
Hapa kwenye
ulevi wa pombe walimuacha kwa sababu alikuwa bado ana vihela hela, hivyo
walimuacha ili hela alizo kuwa amebaki nazo azimalizie kwenye ulevi abaki hana
kitu kabisa. Na kweli baada ya muda mfupi akawa ameishiwa hela. Kichwani
mawazo, kazi hakuna, biashara imekufa, aibu mtaani, maneno yameanza
kuzungumzwa.
Jamaa
akaamua kuingia kwenye ulevi wa gongo ili aweze kusahau matatizo yake. Baada ya
kama mwezi mmoja hivi jamaa akawa mlevi wa kupindukia anashinda kwenye vilabu
vya gongo. Akawa anaonekana hajali tena kama aliwahi kuwa na kazi, biashara na
maisha mazuri.
Wale magwiji
hawakupendezwa na hali hii,kwa sababu wao walitaka kijana huyo baada ya kutiwa
nuksi hiyo auone uchungu wa kuishimaisha ya kilofa na umasikini ulio tukuka na
kibaya zaidi wakamfunga asiondoke kijijini hapo ili wawe wanamuona anavyo
adhirika.
Taarifa za
ulevi wa gongo wa kijana huyo hazikuwafurahisha hata kidogo,.Kwa sababu
zilikuwa na maana mbaya sana katika kamusi yao.
Walicho
kifanya wazee hao wakamtafuta kijana huyo na kumpa
dawa ya
kuacha pombe..
Dawa hii ni
tofauti na ile inayo changanywa na mayai ya ndege mmoja mweusi anaepaa au ile
inayo changanywa na mavi ya ndege mmoja mweupe afugwae.
Hiidawa
inatokana na mizizi ya mti mmoja wa porini wenye jina
linalo
fanana na jina la wilaya moja iliyopo kusini mwa Tanzania. Huwa ni mwiko kwa
mwanamke mjamzito kuuruka mzizi wa mti huu kwa sababu akifanya hivyo, mimba
itaharibika.
Katika
baadhi ya jamii za kiafrika, mtu anapokufa kwa kujiua mwenyewe,maiti yake huwa
haingii ndani na kipande cha mzizi wa mti huu huwa kinachomekwa kwenye makalio
ya mwili huo ili kuvunja roho ya kujiua katika m familia na ukoo huo.
Huwa
unachukuliwa mzizi wa mti huo ambao umekufa wenyewe, kisha unasagwa halafu
anapewa mlevi.
Kijana huyo
alipopewa dawa hiyo alitapika sumu zote na toka
siku hiyo
alichukia kabisa pombe na ulevi wa aina yoyote ile.
Kilicho
fuatia baada ya hapo, kijana huyo akawa anafanya kazi
ambazo
haziendani na elimu yake.
Kwanza akawa
anabeba mizega ya maji, mara anazibua vyoo, mara anauzakaranga ilimradi watu
wamuone anavyo adhirika. Wao hwafaidiki na chochote lakini wanafurahia kumuona
kijana huyo akiwa anateseka na kudhalilika.
Kuhusu
matumizi ya uchawi na ushirikina katika mchezo wa mpira wa miguu, Dokta Mungwa
anasema,mambo hayo siku hizi hayafanyiki kama ilivyo kuwa inafanyika zamani.
Siku hizi mambo yamebadilika tofauti na ilivyo kuwa zamani. Mambo yamebadilika
sana siku hizi. Kwanza siku hizi vijana wanacheza mpira wa kulipwa tofauti na
ilivyo kuwa zamani ambapo watu walikuwa wanacheza mpira wa ridhaa na kwa
mapenzi ya timu husika.
Zama hizo
watu walikuwa wanatumia sana uchawi katika mpira. Kila namba ilikuwa na uchawi
wake na uchawi ulitofautiana kutoka timu moja na nyingine.
Kwa mfano,
kwenye nafasi ya kipa
kipa ilikuwa
kilikuwa kinachukuliwa kipande cha sanda iliyo tumika kumvesha maiti, kisha
linachukuliwa karatasi jeupe ambalo yanaandikwa majina ya wachezaji wote wa
timu pinzani kisha unawekwa unga wa kisiki ambacho watu wakipita njiani
wanajikwaa kwaa na vitu vingine viwili ambavyo sita vitaja hapa. Baada ya hapo
ilishonwa azima ambayo alipewa kipa na kutakiwa kuvaa kwenye mguu au mkono
wowote.
Ndumba hii
iliaminika kumsaidia kipa kuwa na uwezo mkubwa wa kudaka mipira awapo golini na
pia kuwafanya wachezaji wa timu pinzani kuwa wanajikwaa kwaa na kuanguka
wenyewe kila wanapo karibia lango.
Kwa
wachezaji wanao cheza namba 2,3,4 na 5 ilichukuliwa mizizi ya nturantura kisha
zinachongwa mpigi 4 ambazo kila moja itafungwa au kushonwa na nyuzi nyeusi
kisha wanapewa wachezaji wa namba hizo na kuzivaa, baada ya kuzikaanga zote na
majina ya wapinzani kwenye mafuta maalumu pamoja na dawa inaitwa Tunda la Jini
au Tufahal Jinni. Dawa hizo zilimwagiwa kwenye kigae cha chungu kilicho vunjika
wakati kikiwa kimebeba maji yaliyo chotwa kisimani. Baada ya hapo yaliandikwa
majina ya wapinzani wote kwenye sahani maalumu nyeupe kwa kutumia zaafarani
nyekundu na baadae kufutwa kwa kutumia vidole. Kila mchezaji alipewa mpigi 4
ambazo zilifungwa kwenye azima na kuzivaa.
Ama kwa
upande wa viungo na washambuliaji, wao ilichukuliwa mizizi ya miti mitatu
mkuyu, Mzungupori na Mtundaugoro,ambayo ilisagwa na kuchomwa pamoja hadi kuwa
unga au majivu laini sana. Baada ya hapo ulichukuliwa upinde ambao ulitumika
kuua nguruwe pori,upinde huo ulisagwa pia na kuchomwa hadi kuwa majivu,vyote
hivi vilichanganywa na mafuta maalumu na kisha wachezaji hao walipakwa au
kuchanjiwa.
Wakati
mwingine ulitumika uchawi wa kuroga timu pinzani, kufanya wachezaji wote wa
timu pinzani wakose pumzi wakiwa uwanjani, ambapo alikuwa anatumika mnyama
mmoja na kamba maalumu.
Wakati
mwingine mchezaji wa timu moja angeweza kufanya uchawi wakuwaroga wachezaji
wenzake wanao gombania namba na kumfanya aonekane yeye ndio zaidi ya wenzake.
Mfano mshambuliaji aliweza kufanyiwa uchawi, magoli yote afunge yeye mwenyewe
au mafowadi wenzake wafunge kwa kupitia miguu yake. Fowadi huyu alinuiziwa kuwa
goli lolote kutoka kwenye timu yake lisifungwe hadi lipitie kwanza kwenye mguu
wake au kichwa chake.
Miaka hiyo
ya zamani, uchawi na ushirikina kwenye mpira ulifanyika kama sehemu ya burudani
ya mpira. Waganga walitumia michezo ya mpira wa miguu kushindanisha nguvu zao.
Wachezaji
wali waogopa zaidi wachawi kutoka nje ya uwanja kuliko wachawi wa ndani ya
uwanja.
Mchezaji wa
mchangani alikuwa akipata nafasi ya kwenda kucheza kwenye timu kubwa basi
ilifanywa siri hadi atakapo anza kuichezea rasmi timu hiyo kubwa.
Mwishoni mwa
miaka ya themanini, kuna kijana mmoja katika kitongoji kimoja cha kwenye mkoa
mmoja unaopatikana mashariki wa Tanzania alikuwa kiungo mshambuliaji hatari
sana. Alikuwa anachezea timu mmoja iliyo kuwa inashiriki ligi daraja la tatu
kipindi hicho. Basi mabosi wa timu moja kubwa wakamuona, wakawa wamemkubali
sana, wakamfuata kuzungumza nae ili akasajiliwe kwenye timu hiyo kubwa, bila
kuchelewa kijana akakubali na mipango ya kumchukua ikaanza kufanyika.
Alikuwa
anatakiwa akaripoti klabuni siku ya Jumatatu kwa ajili ya kwenda kusaini
mkataba mnono pamoja na kujiunga na wenzake kambini. Baba wa kijana huyo kwa
furaha ya mtoto wake kusajiliwa kwenye timu kubwa akaanza kuwaambia, ndugiu,
jamaa, majirani na marafiki. Habari zikawafikia magwiji na kama ilivyo
tazamiwa,. Hazikuwapendeza. Magwiji wakaunda kamati ya kumuwekea zuio kijana
huyo asiweze kwenda katika timu hiyo kubwa.
Ilikuwa siku
ya Ijumaa, wazee wa mtaa wakamwambia baba wa kijana kuwa wameandaa sherehe
maalumu ya kumuaga na kumpongeza kijana wao kwa sababu ameleta heshima kubwa
sana kwenye mtaa wao. Kijana akatakiwa na yeye kuhudhuria. Baba mtu akakubali
kwenda ili isionekane amekataa kwa sababu anaringa mtoto wake amesajiliwa kwenye
timu kubwa. Kaka wa baba mtu ( Yani baba mkubwa wa kijana yule mchezaji ) nenda
kwenye sherehe ila kijana asiende kwa sababu wanaweza kumlisha uchawi kwenye
chakula atakacho kula. Baba mtu akasema “ Nisipoenda na huyu kijana itaonekana
kijana amedharau wito wa wazee, ngoja niende nae tu, cha msingi sitaruhusu ale
chakula kwenye sahani yake mwenyewe. Nitahakikisha chakula kinaletwa kwenye
sahani ya kula watu wote kwa pamoja na ikiwezekana tule pamoja na wazee walio
tualika “. Kaka mtu akamwambia “ WACHA UPUMBAVU BWANA MDOGO.. DAWA HUWA
ZINANUIZIWA. MNAWEZA KULA WOTE CHAKULA KWENYE SAHANI MOJA LAKINI AKADHURIKA MTU
MMOJA KWA SABABU ANAKUWA AMENUIZIWA MTU HUYO HUYO MMOJA, KWA HIYO CHA MSINGI
HAPA .. KIJANA ASIENDE KABISA. WAAMBIE ANAUMWA NA KICHWA “
Baba wa
kijana hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na ushauri wa kaka ake. Kijana
kweli hakwenda kwenye hiyo sherehe kwa madai kwamba anajisikia kichwa
kinamuuma. Mchana wa siku iliyo fuata sasa yani Jumamosi , kijana akaanza
kulalamika kichwa kinamuuma, kichwa kinamchemka.
“ Baba
kichwa kinauma, baba kichwa kinachemka !”. Inaelezwa kuwa joto la kijana huyo
lilipanda kwa kasi ya ajabu katika namna ya kutatanisha. Inaelezwa zaidi kuwa
kichwa cha kijana kilichemka kiasi kwamba ungeweza kuweka mtungi au sufuria la maji
kichwani kichwani kwa kijana huyo yakachemka ndani ya muda mfupi kwa kiasi
ambacho ungeweza kunyonyolea kuku !
Baba wa
kijana hakuwa na jinsi zaidi kuwahisha kijana wake hospitali. Kufika hospitali
madaktari kumpima wakakuta mtu alisha ondoka duniani toka enzi za Pontyo wa
Pilato.
Nirudi kwa
jamaa anaetaka Sanchez atupiwe uchawi wa kumfanya ashindwe kun'gaa kwenye timu
yake mpya. Mawazo kama hayo yanaweza kukaa na kuishi ndani ya akili za wachawi
tu. Hutakiwi kabisa kuwa na mawazo kama hayo.
Unamchukia
mtu ambae hakujui wala hajui kama unamchukia na aathiriwi na chochote kuhusu
chuki yako. Unadhani nani anae umia hapo kati yako wewe na Sanchez ?
Kumchukia
mtu ambae hakujui wala hajui kama unamchukia, ni sawa na kuwapangisha kwenye
nyumba yako, wapangaji ambao hawakujui na hawajui kama umewapangisha halafu
wewe ndio unawalipa wao kodi. NI uwendawazimu.
Nafsi yako
ni nyumba yako uliyo pewa na Mungu. Ndani ya nafsi yako unatakiwa uwapangishe
wapangaji watakao kulipa kodi nzuri. Pangisha, furaha, amani, upendo,
matumaini, imani nakadhalika. Ukipangisha chuki , husda na choyo, wewe ndio
utakae umia. Utaishia kuvuna magonjwa kama presha, shinikizo la damu au
kiharusi na kuvuta mapepo yatakayo endelea kukuletea nuksi kwenye maisha yako.
Kingine,
unatakiwa kujua kuwa uchawi au uganga ni tofauti na mazingaombwe. Lazima uwe na
sababu ya msingi na yenye akili. Hii ni kwa sababu uchawi ni gharama sana.
Unahitaji vitu vingi ili jambo lililo kusudiwa liweze kutokea.
Ndio maana
basi hata wachawi wenyewe wanapo taka kumroga mtu huwa wanaanza na njia za
kawaida kwanza ambazo hazihusishi uchawi zikishindwa ndio wanaingia vitani
rasmi kwa kuhusisha uchawi.
Kwa mfano
wachawi wanataka kuwatenganisha mke na mume au mtu na mchumba wake. Kwa kuanza
wataanza na umbea kwanza. Wanachukua maneno kwa mwanamke wanapeleka kwa
mwanaume, wanachukua maneno kwa mwanaume wanapeleka kwa mwanamke. Wakiona
mpango wao umeshindikana, hapo ndio wanatumia uchawi.
Ndio maana
miaka ya nyuma watu walio kuwa wanaenda kwa waganga kutafuta suluhisho kwa mambo
ya kipuuzi walikuwa wanaishia “kulaaniwa wao wenyewe “ na waganga hao.
Kwa mfano
kulikuwa na baadhi ya wanaume, anaenda kwa mganga na kusema “ MGANGA NAOMBA
UNIFANYIE DAWA ILI MKE WANGU ASIWE ANANIOMBA HELA YA MATUMIZI. ASAHAU KABISA
KUHUSU KUNIOMBA HELA YA MATUMIZI HADI SIKU ANAINGIA KABURINI “
Mwanaume
kama huyu ni mwanaume asie faa, kwa lugha nyingine anaweza kuitwa “ Khanithi “
. Mwanume wa hivi, kwanza alikuwa analazwa dhakari yake kwa kutumia akili yake
ambayo imelala, halafu anafungwa kuzaa kabisa ili asirithishe upumbavu wake kwa
watoto atakao wazaa... Na mwisho wa siku alitupiwa uchawi unaitwa “ SUNKHWA “
ama “ FUKUZA “ ambao ungemfanya aondoke kabisa kijijini hapo na kwenda kulowea
kusiko julikana. Baadae lingefanyika tambiko maalumu la kutakasa kijiji hicho
dhidi ya najisi ya mwanaume huyo.
Nimetoa
maelezo haya ili kuwasaidia pia baadhi ya mashabiki wa Arsenal ambao wanaweza
kuwa wameumizwa na kuondoka kwa Sanchez na ambao pia wanaweza kuwa na mawazo
kama ya jamaa aliye taka nimroge Sanchez ili asipate mafanikio kwenye timu yake
mpya.
Kama upo
kwenye kundi hilo, huu ni ushauri wangu kwako :
1. JIPE MUDA
UTASAHAU : Hakuna dawa nzuri ya kusahahu kitu au jambo unalo lipenda kama MUDA.
Mwanzoni unaweza kuumia kumuona Sanchez akishangilia baada ya kuifungia timu
yake mpya magoli kwenye mechi mbalimbali. Baada ya muda utazoea na utaona
kawaida kabisa.
2.
USIANGALIE MECHI ZA MAN U : Usiangalie mechi za Man U. Wewe subiri tu kuambiwa
matokeo.
3. JITENGE :
Siku ambayo Arsenal watacheza na Man U usitazame mpira pamoja na jamaa zako
ambao ni mashabiki wa Man U. Nenda kaangalie mpira sehemu ambayo haujulikani.
4. HAMA MTAA
UNAOISHI : Kama unadhani hauwezi kuwakwepa jamaa zako mashabiki wa Man U ambao
watakua wanakuja kukukera wakishangilia namna Sanchez anavyo funga magoli, hama
kabisa mtaa unaoishi/
5. BADILISHA
NAMBA ZAKO ZA SIMU : Kwa sababu jamaa zako watakuwa wanakukera kukupigia simu
kukwaambia kuhusu namna Sanhez anavyo fanya vitu vyake. Badilisha namba zako za
simu ili wasikutafute kabisa.
6. BADILISHA
OFISI AU ACHA KAZI KABISA : Kwa sababu si unasema wafanyakazi wenzako ofisini
watakuwa wanakukera na habari za Sanchez. Basi kama ni mfanyabiashara, tafuta
eneo jipya la biashara, au kama una ofisi yako, tafuta ofisi mpya au kama
umeajiriwa, basi kazi kabisa ili uwe mbali nao.
7. HAMIA MAN
U : Kwa sababu unampenda na unamkubali sana Sanchez na Sanchez ndo hivyo tena
amehamia Man U. Kitu cha kufanya hapo wewe hamia Man U ili ukaendelee
kuburudishwa na uchezaji wake.
8. JIFANYE
HUJUI KAMA SANCHEZ ALIWAHI KUCHEZEA MAN U
9. FANYIWA
TAMBIKO MAALUMU LA KUSAHAU KUHUSU SANCHEZ : Badala ya kuomba Sanchez asahau
magoli, wewe ndio ufanyiwe tambiko maalumu la kusahau kuhusu Sanchez. Ukimuona
Sanchez umuone kama takataka vile. Usikumbuke kama aliwahi kuchezea Arsenal.
10. 8. Kama
unaona ushauri huo hapo juu ni UPUMBAVU basi kumchukia Sanchez kwa sababu
kahamia MAN U pia ni UPUMBAVU ZAIDI.
Kitu kingine
unacho takiwa kufahamu ni kwamba, Sanchez anatafuta maisha yake. Man U wamempa
ofa ya kumlipa Pauni 500,000/= kwa wiki ambacho ni kiasi kikubwa sana cha pesa.
Ni mpumbavu tu ndio anae weza kukataa ofa nzuri kama hiyo. HAKUNA MTU ASIEPENDA
PESA. HATA WAZAZI WENU WANAWEZA KUWA WANAWAPENDA SAWA SAWA WAKATI MKIWA WATOTO
WADOGO. LAKINI PINDI MTAKAPO ANZA KUJITEGEMEA WATAMPENDA NA KUMBARIKI ZAIDI
MTOTO WAO ANAEWAJALI NA KUWATUNZA KWA KUWAPA PESA KULIKO WEWE AMBAE PESA ZAKO
UNATUMIA KUFANYA STAREHE NA HUPELEKI MATUNZO KWA WAZAZI WAKO.
0 Comments