Chama cha
Mawakili Tanganyika (TLS) kimesema kimefanikiwa kukusanya Sh138 milioni
kugharamia matibabu ya Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya
Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji.
Taarifa
iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa TLS, Godwin Ngwilimi amesema kiasi hicho
wamekipata kutoka kwa watu mbalimbali walijiotolea kuchangia wa ndani na nje ya
nchi wakiwemo wanachama wa chama hicho.
Kuhusu
mchanganuo wa fedha hizo, Ngwilimi amesema kimetumika kulipa gharama za
matibabu ya Lissu katika Hospitali ya Nairobi, Leuven na visa kwa watu watatu
wakiwa nchini Ubelgiji.
Ngwilimi
ametoa shukuran kwa wale wote waliojitokeza kuchangia matibabu ya Lissu ambaye
pia ni mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chadema.
Lissu
aliyeshambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017
akiwa katika makazi yake mjini Dodoma ambapo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya
Dodoma na usiku wa siku hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alikolazwa hadi
Januari 6 baada ya kahamishiwa Leaven, Ubelgiji kwa mazoezi ya viungo na
saikolojia.
0 Comments