Kiongozi wa
upinzani Raila Odinga (NASA) ameapishwa kuwa ‘Rais wa Wananchi’ wa Kenya licha
ya kugomea uchaguzi mkuu wa marudio nchini humo.
Raila Odinga
amefika leo katika Uwanja wa Uhuru Park pamoja na viongozi wengine wakuu wa
NASA akiwemo Moses Wetangula na Musalia Mudavadi na kujiapisha akishika Biblia.
Aidha,
mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa Chama Cha Wiper hakuwepo wakati wa
kuapishwa kutokana na kuhofia kukamatwa, ambapo Odinga amesema ataapishwa
baadaye.
“Odinga
amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya, hatua ya leo ni kuelekea kutoa
udikteta na kuleta demokrasia Kenya, maelekezo mengine mtayapata baadae,”
alisema Odinga baada ya kuapishwa. Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari
cha KTN kwamba shughuli hio ‘ si mapinduzi ya serikali’
Raila
aligomea uchaguzi huo kwa sababu za kusema kuwa tume ya Uchaguzi nchini humo si
ya Uhuru na haki. Uchaguzi huo wa marudio ulikuja baada ya Mahakama ikiongozwa
na Jaji Maraga kutengua Uchaguzi wa awali uliofanyika 8 Agosti.
Katika
uchaguzi huo wa Oktoba, Rais Kenyatta alitangazwa mshindi akiwa na kura 7.5
milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizokuwa zimepigwa.
Waliojitokeza
kushiriki uchaguzi huo walikuwa 39% kati ya waliojiandikisha kupiga kura.
Kenyatta aliapishwa kuwa Rais wa Kenya baada ya uchaguzi wa marudio mnamo
tarehe 28/11/2017
0 Comments