
Muimbaji
nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae,
Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14
tangu waachie kibao kipya.
Wawili hao
walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya
Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao wanaopendwa sana
kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.
Naibu Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bi. Juliana Shonza aliwakutanisha na
uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena
kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio
hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Wameanza kwa
kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana na
kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa Tanzania
umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.
“Miaka 14 si
mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliyamiss, nimemiss vitu vingi,
picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia
nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa photoshoot.
Kwa
kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za
zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi
ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.
Kwenye
photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu Seya na Papii
Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.
Unaweza
kuangalia video ya behind the scenes ya upigaji picha kwa kufuata link hii
>> https://youtu.be/h-Kdp87now4
0 Comments