Nyumba ya
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila imechomwa moto katika
shambulizi linaloshukiwa kufanywa na waasi, ambapo askari mmoja aliuwa.
Tukio hilo
limetokea Desemba 25, 2017, ambapo taarifa zinasema kuwa waasi wa kundi
lijulikanalo Mai Mai walijaribu kuiba mali kutoka makazi hayo ya rais yaliyoko
eneo la Musienene, katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.
Wakati wa
tukio Rais Kabila hakuwa kwenye nyumba hiyo ambayo iko kijijini maili 1,680
Mashariki mwa mji wa Kinshasa, huku kundi la Mai Mai na kundi la waasi wa ADF
wakiwa washukiwa wa kwanza juu ya tukio hilo.
Hivi
karibuni Rais Kabila amekuwa akipingwa na wanasiasa mbali mbali kwa kitendo
chake cha kutaka kugombea nafasi ya urais kwa muhula mwingine.
0 Comments