
Mwimbaji kutoka WCB ambaye anafanya vizuri katika mziki wa
Bongofleva Diamond Platnumz kupitia Clouds 360 ya Clouds TV amemtambulisha
msanii mpya ambaye atakuwa mmoja kati ya
wasanii wanaounda kundi hilo.
Katika utambulisho huo Diamond amesema kuwa ana wajibu
mkubwa wa kuwasaidia wengine kwa kuwa hata yeye alisaidiwa ndiyo maana amefikia
hatua hiyo aliyofikiwa.
“Ujio wangu hapa leo ni kwa ajili ya kumtambulisha kijana
wetu mwingine kama sehemu ya kuwasaidia wengine. Nawashukuru sana Clouds Media
kuwa kama daraja kuwasaidia wengine. Kama nisingesaidiwa nisingefika hapa.
Inapotokea mtu anasaidiwa nashiriki kwa kidogo nilichonacho kwa sababu mimi
nisingesaidiwa nisingefika hapa”.

0 Comments