Follow us

SIMBA KAMILI KUWAKABILI YANGA KWA MKAPA

Tangazo

 

SIMBA KAMILI KUWAKABILI YANGA KWA MKAPA

SHOMARI Kapombe, beki wa kupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Simba ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga.

Aprili 20 2024 mchezo wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mzunguko wa pili kwa timu hizo kukutana.

Ipo wazi kwamba kwenye mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga na mfungajiwa bao la kwanza kwa upande wa Yanga alikuwa ni Kennedy Musonda bao lile la Simba lilifungwa na Kibu Dennis.

Kapombe amesema: “Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Yanga na wachezaji tupo tayari kuona kwamba tunapata matokeo,makosa yaliyopita tumefanyia kazi,”.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Post a Comment

0 Comments