Tangazo
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ WallaceKaria, amezipongeza Klabu za Simba na Young Africans kwa kufanikiwa kutingahatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akisema wameipa sifa nchi, nakwalke binafsi wamemheshimisha mbele ya viongozi wa mashirikisho mengine Afrikana dunia lakini akitoa siri ya mafanikio hayo.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo, timu za
Simba na Young Africans zimetinga kwa pamoja hatua ya Robo Fainali huku
Tanzania ikiwa nchi pekee iliyoingiza timu mbili katika hatua hiyo.
Mara nyingi imezoeleka kuona nchi za Kaskazini maarufu nchi
za Kiarabu hususan Misri, Morocco na Tunisia zikiingiza timu mbili katika hatua
hiyo, lakini safari hii ni Tanzania pekee iliyofanikiwa kufanya hivyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Karia, amesema hayo yoteyametokana na kuigeuza ligi ya Tanzania kutoka kuwa ya ridhaa na kuwa yakulipwa na ya kibiashara zaidi, hali iliyosababisha kuja kwa wachezaji wengi wakigeni na wenye ubora mkubwa.
“Nazipongeza Klabu Simba na Young Africans, kuanzia viongozi
na wachezaji wao, kuingia kwao hatua ya Robo Fainali kumeiheshimisha za nchini
yetu, ni Tanzania pekee iliyoingiza timu mbili msimu huu, wameniheshimisha mimi
kama Rais wa TFF mbele ya viongozi wenzangu na Mashirikisho ya Soka Afrika na
duniani kwa jumla.
“Pia napeleka pongezi zangu kwa wachezaji wa kigeni wa Simbana Young Africans kwani wamezifikisha timu hizo hapo na wamewabadilisha hatawachezaji wetu wazawa.”
Amesema awali walipoweka idadi ya wachezaji 12 wa kigeni
walipata upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wadau wa michezo, lakini kwa sasa
Kitanzania,” alisema Karia. matunda yake yanaonekana.
“Tuliruhusu wachezaji 12 wa kigeni ili mradi tu tukawekavigezo wawe wa viwango gani, tulipata upinzani mkali, lakini leo tunaona, ni haohao kwa kiasi kikubwa wamezisaidia timu hizi za Tanzania ambapo sidhani kamatungekuwa na Watanzania watupu tungeweza.
“Lakini hawa wachezaji wa kigeni wamesaidia hata
kuwaimarisha wachezaji wetu kwa sababu kila wiki wanacheza nao hapa kwenye
ligi, kwa hiyo hata wakichaguliwa kwenye timu ya taifa wanakuwa hawana woga nao
kwa kuwa wamewazoea,” amesema Karia.
Amekumbushia michuano ya AFCON 2023 iliyoisha hivi karibuninchini Ivory Coast, ambapo Tanzania ilikuwa kwenye kundi moja na Zambia,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Morocco kuwa Taifa Stars haikufanya vibayasana na nusura iende hatua ya 16 bora, kwa sababu Stars, ilikuwa kundi lenyetimu zenye wachezaji wanaowafahamu.
“Wachezaji wetu waliihofia Morocco tu, lakini siyo Zambiakwa sababu ilikuwa na wachezaji wanaocheza nao kila wiki (Clatous Chama naKennedy Musonda), na DR Congo (Henock Inonga), na hiyo ndiyo faida ya kuwa nawachezaji wa kigeni, inawaimarisha hata wachezaji wa Kitanzania kwenye timuyetu wa Taifa Stars,” amesema.
Aidha, aliwapongeza pia wadhamini mbalimbali wa ligi ambaowataonyesha mechi zote 240 za Ligi Kuu, akisema hayo ni maendeleo makubwa yasoka kipindi cha uongozi wake, ambapo sasa wachezaji wa timu zote 16 za LigiKuu na wa chini ya miaka 20 wanalipwa mishahara.
0 Comments