Follow us

Tangazo

 


MOTO WA FEITOTO WAONGEZEKA, WAKATI AZAM IKIPETA.

KIUNGOmzawa mali ya Azam FC Feisal Salum MWENYE jumla ya mabao 11 katika orodha yawatupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara anazidi kuonyesha ubora wake kwa vitendouwanjani.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Machi 3 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 4-1 Dodoma Jiji na Fei alitupia mabao mawili.

Mabaoya Azam FC yalifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 28, Feisal dakika ya 63, 64,Kipre Junior dakika ya 69 na Emmanuel Martin alifunga kwa mkwaju wa penaltidakika ya 84.

>>>KAULI YA FEI TOTO KUHUSU KASI YAKE ILIVYOONGEZEKA HII >>>>HAPA

Ushindi huo unaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 43 kibindoni msimu wa 2023/24 sawa na vinara Yanga wakitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kiungohuyo anaongoza chati ya watupiaji kwa sasa akifuatiwa na Aziz KI wa Yangamwenye mabao 10.

Post a Comment

0 Comments