BEKI mwili
nyumba wa Simba, Mohammed Ouattara, ameona isiwe shida na kufikia makubaliano
mazuri na klabu hiyo, ya kuvunja mkataba ili aondoke hapo Msimbazi.
Outtara ni
kati ya wachezaji waliosajiliwa na Simba katika usajili mkubwa msimu huu
akitokea Al Hilal ya nchini Sudan akisaini mkataba wa miaka miwili.
Beki huyo
alisajiliwa na Simba kwa ajili ya kuiboresha safu ya ulinzi ya timu hiyo,
lakini akashindwa na kufikia maamuzi hayo ya kuondoka.
Kwa mujibu
wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Simba, Ouattara
amekubali kuondoka Simba kwa makubaliano ya pande zote mbili kufikia muafaka.
Chanzo hicho
kilisema uongozi wa Simba hivi sasa upo katika mazungumzo na baadhi ya mabeki
wa kati watakaokuja kuchukua nafasi yake na kucheza pamoja na Mkongomani,
Hennock Inonga.
Kiliongeza
kuwa, sababu kubwa ya beki huyo kuondoka, ni kukosa nafasi ya kudumu ya kucheza
katika kikosi cha kwanza, licha ya kuamini kiwango chake alichonacho yeye.
“Mazungumzo
ya pande zote mbili baina ya beki Ouattara na Uongozi wa Simba yamefikia katika
sehemu nzuri ya yeye kuondoka hapo baada yeye mwenyewe kuridhia.
“Siku yoyote
kuanzia jana (Jumatano) alitarajiwa kupanda ndege kurejea nyumbani kwao huku
akiweka mikakati ya kwenda kutafuta changamoto
sehemu nyingine.
“Ouattara
hakuwa na msimu mzuri tangu ajiunge na Simba baada ya majeraha kumuandama mara
kwa mara huku akipoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza,” kilisema chanzo
hicho.
Meneja wa
Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alizungumzia hilo kwa kusema: “Kila
kitu kinachohusiana na usajili kwa hivi sasa kipo kwa kocha wetu Robertinho
(Roberto Oliveira), na hivi karibuni kitawekwa wazi kila kitu baada ya taratibu
kukamilika za kusajili na kuacha wale wachezaji wanaotakiwa kuachwa.”
0 Comments