Follow us

YANGA YAIPIGA MKWARA MWINGINE SIMBA

Tangazo

 

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kushindwa kupata ushindi dhidi ya watani zao wa jadi ni mwanzo wa kulipa kisasi wakikutana kwenye mchezo wa ligi.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Agosti 13 ilishuhudia ikivuliwa taji la Ngao ya Jamii na watani wa Jadi Simba waliopata ushindi wa penalti 3-1 kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wakikutana kwenye ligi hakuna mshindi anayepatikana kwa penalti kama ilivyokuwa kwenye mchezo wao uliopita.

“Fainali ni fainali na wachezaji wetu wamecheza fainali kubwa kwenye mashindano ya kimataifa ambayo ilikuwa hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika hivyo uzoefu upo kwa ushindi waliopata tunawapongeza.

“Lakini ninapeda kusema kuwa wachezaji walionyesha uwezo mkubwa tunakwenda kwenye ligi na huku tukikutana hakuna penalti huo ni uzuri wanapaswa wasijisahau katika hilo tupo imara,” amesema Kamwe.

Mchezo wa Kariakoo Dabi kwa msimu wa 2023/24 unatarajiwa kuwa Novemba 5 2023 na Simba watakuwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa.


Post a Comment

0 Comments