KUTOKANA na usajili waliofanya na
ubora wa kikosi kwa msimu wa 2023/24, mashabiki wa Simba wameomba kupewa sumu
ikiwa tu timu hiyo haitatinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23
watani zao wa jadi Yanga walitinga hatua ya fainali katika Kombe la Shirikisho
Afrika.
Pia mgeni rasmi, Rais Samia Suluhu
aliweka wazi kuwa anatambua mafanikio ya Simba kugotea hatua ya robo fainali
Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga kufika hatua ya fainali.
Samia aliongeza kuwa ni muhimu timu
zote kushirikiana iwe ni Simba, Yanga, Azam FC na Singida Fountain Gate
inapofika suala la mashindano ya kimataifa.
Simba inayonolewa na Kocha Mkuu,
Robertinho Oliveira inashiriki mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka
Afrika, (CAF) msimu wa 2022/23 iligotea hatua ya robo fainali.
Katika kilele cha Simba Day, Agosti 6
miongoni mwa mabango ya mashabiki yaliyozua gumzo ni pamoja na lile
lililosomeka namna hii: “Kwa Simba hii tusipofika nusu fainali Club bingwa
nipewe sumu nife.”
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo
ndani ya kikosi cha Simba msimu ujao ni Luis Miquissone, Clatous Chama, Kibu
Dennis, Shomari Kapombe na John Bocco.
0 Comments