Arusha, Agosti 21, 2023
Askofu Mkuu wa Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo, amesema kuwa kanisa
lake lina imani na namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan analisimamia suala la
uwekezaji kwenye bandari na kumpongeza Rais kwa uongozi wake wenye hekima.
Kanisa la KKKT limesema
kuwa linamuunga mkono Rais Samia na linaunga mkono uwekezaji nchini.
KKKT pia imekemea watu
wanaotaka kuligawa taifa kupitia kwa mjadala unaoendelea wa bandari kwa maslahi
yao binafsi ya kidini, kisiasa na kiuchumi.
Zifuatazo ni kauli 10
nzito zilizotolewa na KKKT kupitia kwa Askofu Mkuu Dk Shoo:
1. "Lipo hili la
DP World Mheshimiwa (Rais). Kwanza naomba lieleweke wazi kwamba kanisa linaunga
mkono uwekezaji. Hatupingi uwekezaji Mheshimiwa Rais"
2. "Tunajua wewe
(Rais) kwenye nia yako unataka wawekezaji"
3. "Sisi viongozi
wa dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni kabisa mwa
jambo hili (mjadala wa DP World) na kwa uungwana wako na kwa unyenyekevu
ulionao na utayari wa kusikiliza, ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama
taasisi na viongozi wakuu wa dini katika nchi yetu ya Tanzania. Madhehebu yote
ya Kikristo, tukiwa CCT, tukiwa TEC na tukiwa BAKWATA. Mimi nakumbuka jinsi
ulivyotupokea, ukatusikiliza. Ukapokea maoni yetu na ushauri wetu viongozi wa dini
na ukaahidi kuwa maoni na ushauri hayo utayapeleka kwa wataalamu na kufanyiwa
kazi kwa uzito kwa maslahi mapana ya taifa"
4. "Tuna imani na
wewe Mheshimiwa Rais"
5. "Tunakuamini
Mheshimiwa Rais na tunaamini kwamba ukisema taasisi zako na vyombo vyako
vitafanyia kazi jambo hili (ushauri wa viongozi wa dini), unamaanisha
hivyo"
6. "Katika jambo
hili tunaelekea mahali ambapo tunataka kugawanyika kabisa, wengine wanatumia
sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na maslahi ya
kiuchumi"
7. "Namshukuru
Mungu amekujaalia (Rais Samia) hekima katika hili (mjadala wa bandari) kama
Mama na Kiongozi, umekaa kimya"
8. "Jambo hili (bandari) linahitaji hekima kubwa la kuliendea na sisi tunaendelea kukuombea (Rais) kwa Mungu ili hekima yote itumike katika kuweza kuleta muafaka wa jambo hili pasipo kutumika kama kitu cha kuchochea wananchi kwa watu wenye malengo yao mengine"
9. "Mheshimiwa
Rais kanisa liko pamoja na wewe"
10. "Tutaendelea
kukuombea (Rais) na kukuunga mkono
katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu kwa maslahi mapana ya nchi
yetu"
Dkt Shoo alitoa kauli
hizo leo jijini Arusha mbele ya Rais Samia kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya
KKKT.
0 Comments