Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud
Yassin akikabidhi kiasi Cha Tsh Milioni 2 Kwa uongozi wa Timu ya Mkwawa Queens
inayocheza Ligi kuu ya Soka la wanawake Tanzania inayotarajia kusafiri jumapili
kwenda Dar,Kucheza na Simba Queens kiasi Cha TshMilioni 3.4 zinahitajika ambazo
zilikuwa zikihitajika Kwa ajili ya safari hiyo .
Akikabidhi msaada huo Leo Kwa uongozi
wa timu hiyo ,Yassin alisema chama Cha Mapinduzi kinatambua mchango mkubwa wa
Timu ya Mkwawa Queens na Timu nyingine Katika michezo na kuwa kutokana na
changamoto ya timu hiyo .
Hivyo alisema Katika kuunga mkono
jitihada za Timu hiyo na jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Katika
kuendelea michezo nchini wao kama CCM mkoa wa Iringa wataendelea kuuunga mkono
jitihada hizo ikiwa ni pamoja na kusaidia sekta ya michezo ndani ya mkoa wa
Iringa.
Alisema jitihada za Mkwawa Queens
wanaziona na kuwa ili Timu hiyo kutimiza vema majukumu yake ni vema wadau
kuendelea kuunga mkono Timu zote ndani ya mkoa .
"Niwapongeze Sana Uongozi wa
Mkwawa Queens Kwa kuendelea kuwakilisha mkoa Katika soka la wanawake na sisi
kama chama tupo pamoja "
Aidha Yassin alimpongeza mkuu wa mkoa
wa Iringa Halima Dendego pamoja na Viongozi wengine wa mkoa huo Kwa kuendelea
kusaidia Timu .
Afisa habari wa Mkwawa Queens Francis
Godwin alipongeza mchango huo wa chama na kuwa huo ni mchango mkubwa Kwa Timu
kupokea .
Alisema Kwa Sasa Timu hiyo inasafari
ya kwenda Dar es salaam kucheza na Simba Queens siku ya Jumanne na kuwa timu
itaondoka Iringa Jumapili safari ambayo itaigharimu Timu Tsh Milioni 3.4 baada
ya hapo inajiandaa Kwa mchezo wake Dodoma na Mkoani Lindi ambako ili
kufanikisha Mzunguko uliobaki zaidi ya Tsh Milioni 10 zinahitajika .
Hivyo aliwaomba wadau kuendelea
kuisaidia Timu hiyo na kumpongeza jitihada za Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima
Dendego na uongozi wa CCM mkoa chini ya Mwenyekiti Daud Yassin na wote ambao
wameendelea kuichangia Timu hiyo .
Godwin pia alimpongeza mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati Kwa mchango wake wa Tsh 200,000 na wote
wanaondelea kujitolea Kwa ajili ya Timu akiwemo katibu wa Chadema Kanda ya
Kaskazin Jackson Mnyawami kuchangia Timu namba hii 0715621222 jina la mpokeaji
Maryam Swaleh
0 Comments