Msanii wa
muziki kutoka nchini Uganda, Radio amefariki dunia.
Msanii huyo
ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel, tangu January 23 mwaka huu
hali yake ilikuwa ikiripotiwa kuwa mbaya kufuatia majereha aliyoyapata kutokana
na ugomvi wa klabu.
Hapo jana
Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Milioni 30 kwa ajili ya matibabu ya
msanii huyo, pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya
kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika February 4 mwaka huu katika kanisa la
Light the World.
0 Comments