Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa ndege jijini
Brussels, nchini Ubelgiji ambapo amepelekwa kwa ajili ya awamu ya tatu ya
matibabu yake yatakayohusisha mazoezi ya viungo.
Tundu Lissu
amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya
alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa, kutokana
na kushambuliwa kwa risasi.
Mbunge Tundu
Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa
kwa risasi na watu wasiojulikana, alipokuwa akitokea Bungeni, majira ya saa 7
mchana, karibu na nyumbani kwake Area D, Mjini Dodoma.
Kwa Mujibu
wa taarifa ya madaktari waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa jumla ya risasi 16
zilimpata Tundu Lissu mwilini mwake, na wamefanikiwa kuzitoa, isipokuwa moja
ambayo iko nyuma ya uti wa mgongo wake.
Tundu Lissu
alieleza kuwa wataalamu na madaktari wake walishauri kuwa risasi hiyo ni hatari
zaidi kama ikitolewa kuliko ikibaki ndani ya mwili wake, kutokana na eneo
ilipokwama.
=>Picha
za Mbunge Tundu lissu alipowasili jijini Brussels kwa ajili ya matibabu zaidi
0 Comments