Mbunge wa
Ruaraka Tom J Kajwang’, ambaye alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano
wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park Jumanne amekamatwa.
Mbunge huyo
amekamatwa leo Jumatano mchana na maofisa wa polisi ambao hawakuwa wamevalia
sare nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi.
Alikamatwa
muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga
kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara
yao na posho.
Kajwang’ na
mwanasheria mwingine Miguna Miguna, ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa matukio
ya kwenye viwanja vya Uhuru Park yaliyomalizikia kwa “kuapishwa” Odinga kama
‘rais wa watu’.
Wakati wa
sherehe za kiapo Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi na alishangiliwa sana na
wafuasi wa Nasa.
Odinga
alikula “kiapo” huku Kajwang’ akiwa amesimama nyuma yake japokuwa wajibu wake
katika tukio hilo bado haujafahamika.
0 Comments