Raia wa
Liberia wanasubiria kwa hamu tukio hilo la kuapishwa kwa Rais wao George Opong
Weah,ambapo wamekesha katika uwanja wa mpira wa taifa,mahala ambapo leo
historia ya mwanasoka huyo inajiandika upya kutoka kung'ara katika soka na
hatimaye kuingia katika uga wa siasa kuwa rais wa taifa hilo lenye historia ya
milima na mabonde kisiasa.
George Weah,
maisha yake ya utoto,yalikuwa katika mazingira duni katika mji mkuuwa Liberia
Liberia Monrovia, alipata mafanikio makubwa katika medali ya soka na kufanikiwa
kuchezea timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Chelsea na AC milan.
Ni Muafrika
pekee kuwahi kushinda tuzo mchezaji bora wa FIFA na tuzo ya Ballon.
Weah
aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa
maseneter katika bunge la Liberia.
Aligombea
urais mwaka 2005 ,na Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza
katika uchaguzi huo lakini kashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake
ilisusia kushiriki katika duru ya pili.
Aliyewahi
kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco inayocheza ligi kuu ya
Ufaransa Arsernal Wenga amealikwa na atakuwepo katika uapisho huo.
Meneja huyo
wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza Ligi Kuu ya
Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja
mchezaji huyo angekuwa rais.
0 Comments