Mwanamke
mmoja ajulikanaye kama Sandhya Rani mwenye umri wa miaka 25 huko Kusini mwa
nchini India ameuawa kwa kuchomwa moto na mpenzi wake baada ya kukataa
kuchumbiwa naye.
Kwa mujibu
wa Jeshi la Polisi katika jimbo hilo, mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliona
mwanaume huyo akifuata mwanamke huyo na wakaanza kuzungumza kwa kubishana na
ndipo mwanaume huyo alipochukua mafuta ya taa aliyokuwa ametembea nayo na
kummwagia binti huyo kisha kumuwasha moto.
Inaelezwa
kuwa watu walijaribu kumwokoa binti huyo lakini alikuwa ameungua sana na
alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali.
Inaelezwa
pia kuwa wawili hao wamewahi kufanya kazi ofisi moja. Polisi jimboni humo
tayari wamemkamata mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina la Karthika Vanga.
0 Comments