
Askari wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU) leo wamelazimika kuingilia kati kutuliza vurugu
zilizoazishwa na abiria 75 waliokosa usafiri wa ndege ya kampuni ya FastJet
kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kutokana na hitilafu za kiufundi.
Abiria hao
waliokaa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 3:00 asubuhi walipotakiwa
kusafiri hadi saa 7:00 mchana, walianzisha vurugu kushinikiza kupatiwa usafiri.
Akizungumzia
kadhia hiyo, Meneja wa FastJet Mkoa wa Mwanza, Ezekiel Manyiga amesema ndege
iliyotakiwa kusafirisha abiria hao haikufika kutoka jijini Dar es Salaam kutokana
na kupata hitilafu ya kiufundi.
“Hata abiria
waliotakiwa kusafiri kutoka Dar es Salaam kuja Mwanza hawajafika hadi sasa;
tunafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kutatua tatizo hili,” amesema Manyiga
Ilipofika
saa 7:00 mchana jana, uongozi wa kampuni hiyo ulifikia uamuzi wa kuwarejeshea
nauli abiria waliokuwa tayari kupokea fedha zao ili kutafuta usafiri mwingine
pamoja na Sh30, 000 ya kujikimu kwa kila abiria aliyekosa usafiri.
“Watakaokuwa
tayari kusubiri ndege yetu watalazimika kusafiri kesho (Jumatano) kwa sababu
ndege tayari imejaa,” amesema Manyiga

0 Comments